Kundi la Aqmi lakiri kuwaua wanajeshi 11 nchini Algeria
Kundi la wanamgambo wa kislamu lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda Aqmi, limekiri kutekeleza aprili 19 shambulio dhidi ya msafara wa magari ya jeshi. Kundi hilo limethibitisha shambulio hilo katika tangazo ambalo limetoa leo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi ziliyotolewa, shambulio hilo liligharimu maisha ya wanajeshi 11.
Imechapishwa:
Usiku wa tarehe 19 aprili, wanamgambo wa kundi hilo la Aqmi lenye mafungamano na kundi la Al Qaeda lilitekeleza shambulio la kuvizia dhidi ya msafara wa magari ya jeshi katika eneo la boudrarène katika mji wa Kabylie, mashariki mwa mji wa Alger.
Tangazo hilo limefahamisha kwamba wanajeshi zaidi ya thelathini ndio waliyouawa katika shambulio hilo na wengine wengi walijeruhiwa , huku kundi hilo la Aqmi likibaini kwamba lilipoteza mpiganaji wake mmoja.
Shambulio hilo liliotekelezwa baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliyofanyika aprili 17 dhidi ya wanajeshi waliokua wakilinda usalama wa uchaguzi,ulisababisha hali ya taharuki katika taifa la Algeria, ambalo katika miaka ya 1990 lilikumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi ziliyotolewa baada ya shambulio hilo, wanajeshi 11 waliuawa na wengine watanu walijeruhiwa vikali, huku waasi watatu wakiwa waliuawa.
Aqmi, kwa upande wake imehakikisha kwamba mmoja miongoni mwa wapiganaji wake , ambaye anajulikana kwa jina la Abu Anas, mkaazi wa Monstaganem (kaskazini magharibi mwa Algeria).
Wapiganaji wa kundi la Al-Tawhid Wal Jihad wanaojulikana kwa jina la “Simba” walijilipiza kisase “kwa ndugu yao aliyeuawa kikatili”, limemalizia tangazo hilo.