Pata taarifa kuu
ALGERIA-Uchaguzi

Bouteflika ashinda uraisi kwa awamu ya nne,wapinzani wapinga matokeo

Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ameshinda kwa mara nyingine uchaguzi mkuu nchini humo huku wagombea wa upinzani wakiyakataa matokeo.

Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika
Raisi wa Algeria Abdelaziz Bouteflika
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya ndani nchini Algeria Tayeb Belaiz ameeleza kuwa Raisi huyo ambaye kwa sasa anamatatizo ya kiafya aliibuka na ushindi wa asilimia 81.53 ya kura zote ikilinganishwa na mpinzani wake wa karibu na waziri mkuu wa zamani Ali Benflis, aliyepata asilimia 12.18.

Belaiz alisisitiza kuwa watu wamemchagua kwa uhuru katika mazingira ya uwazi na halisi.

Bouteflika, mwenye umri wa miaka 77, alishika madaraka kwa mara ya kwanza mwaka 1999 na kuchaguliwa tena mwaka 2004 na 2009 baada ya kufanya mabadiliko ya katiba yaliyomruhusu kugombea tena, alipewa nafasi kubwa nchini humo kutokana na kuchangia kukomesha mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1990 yaliyosababisha vifo takribani laki mbili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.