Pata taarifa kuu
ALGERIA-BOUTEFLIKA-AFYA

Algeria: rais Bouteflika alazwa hosptalini

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Algeria, rais wa Algeria, Abdelziz Bouteflika anasadikiwa kuwa amelazwa hospitalini tangu Alhamisi Novemba 13 katika kliniki ya Grenoble, kusini mashariki mwa Ufaransa. Vyanzo vingine kutoka Algiers vinathibitisha kuwa rais Bouteflika hajaondoka Algeria.

Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwa muhula wake wa nne, Aprili 28 mwaka 2014.
Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika wakati wa kuapishwa kwa muhula wake wa nne, Aprili 28 mwaka 2014. REUTERS/Louafi Larbi
Matangazo ya kibiashara

Inadhaniwa kuwa rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika huenda ameruhusiwa Novemba 13 kulazwa katika klinikiya Grenoble. Gazeti “Le Dauphiné Libéré”,limethibitisha kwamba rais Bouteflika ameruhusiwa kulazwa katika idara ya maradhi ya moyo na mishipa. Daima kulingana na habari ziliyochapishwa kwenye gazeti hilo, "mkuu wa idara ya magonjwa ya moyo na mishipa ambapo Abdelaziz Bouteflika amelazwa wamekua wakijitahidi kufanya kiliyo chini ya uwezo wao tangu miezi miwili iliyopita ili Bouteflika aweze kuwasili katika kliniki hiyo ya Grenoble.

Vyanzo vya polisi vimethibitisha taarifa hiyo, wakati ambapo vyanzo vingine Algiers vimethibitisha kwamba rais Bouteflika hajaondoka nchini. Ikulu ya Algiers imebaini kwamba tangazo litatolewa Ijumaa jioni Novemba 14.

Kudhohofika kwa afya ya rais Bouteflika kumezua uvumi nchini Algeria. Rais Bouteflika alilazwa hospitalini mwaka uliyopita katika mji wa Val de Grâce kufuatia kiharusi.

Hayo yakijiri rais Bouteflika alifanyiwa upasuaji mwezi Novemba mwaka 2005 katika hospitali hiyo ya Paris kwa kidonda tumbo, kulingana na kadi rasmi ya afya aliyopewa baada ya kutoka hospitali. Rais Bouteflika aliendelea kulazwa hospitalini miaka ya 2006 na 2011 mjini Paris, Ufaransa.

Abdelaziz Bouteflika, mwenye umri wa miaka 77, ni rais ambaye anashikilia rekodi ya kuwa madarakani kwa muda mrefu nchini Algeria. Aliingia madarakani tangu Aprili 27 mwaka 1999.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.