Pata taarifa kuu
ALGERIA-NIGER-UHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji haramu 500 wakamatwa Algeria

Wizara ya ulinzi ya Algeria imetangaza Jumapili mwishoni mwa juma hili kwamba wahamiaji haramu walikamwa Jumamosi Aprili 4, katika mikoa ya Tamanrasset na In Guezzam, karibu na mpaka na Niger.

Raia wa Niger karibu na soko la Boufarik, Algeria, Mei 2014.
Raia wa Niger karibu na soko la Boufarik, Algeria, Mei 2014. AFP PHOTO/FAROUK BATICHE
Matangazo ya kibiashara

Opereshini hii inahusiana na zoezi la wahamiaji haramu wa Niger, ambayo Algiers na Niamey wanaanda tangu mwezi Desemba mwaka 2014.

Jeshi la Algeria limethibitisha kwamba watu 496 wamekamtwa. Watu hao ni kutoka mataifa tofauti ya Afrika. Serikali ya Algeria imesema kwamba watu hao waliingia nchini humo kinyume cha sheria.

Kwa mujibu wa mashahidi, vikosi vya usalama vimezingira maeneo kadhaa ya mkoa wa Tamanrasset, na kusababisha hali ya taharuki.

Watu hao waliokamatwa wamefanyiwa uchunguzi. watu ambao si raia wa Niger wameachiliwa.

Wakati huohuo serikali ya Algeria imetangaza kwamba imeanzisha operesheni ya kuwarejesha makwao wahamiaji haramu kutoka Niger. Algeria imesema kwamba operesheni hio iliianza tangu mwezi Desemba mwaka 2014.

Juma moja lililopita opereshni kama hiyo iliendeshwa katika mji wa Oran. Miezi mitatu iliyopita, watu takribani 2,500 walisafirishwa hadi katika mji wa Agadez, kwa makubaliano na serikali ya Niger.

Viongozi wa Algeria wamesema wakisisitiza kwamba zoezi hilo linafanywa kwa makubaliano na wahamiaji wenyewe, ikimaanisha kuwa wahamiaji hao haramu kutoka Niger wamekubali kurejea makwao kwa hiari yao. Lengo la serikali ya Algeria ni kuwasafirisha wahamiaji haramu 3000 mpaka Agadez. Hata hivyo wahamiaji haramu waliofurushwa Algeria wamekua wakirejea nchini humo.

Mwezi Mei mwaka 2014, idadi kubwa ya wahamiaji haramu kutoka nchi za kusini mwa Sahara, hususan Niger waliingia nchini Algeria na kusababisha hali ya sintofahamu. Vyombo vya habari, hususan magazeti vilichapisha wakati huo taarifa mbalimbali kuhusu wimbi hilo la wakimbizi na kupelekea serikali kupatwa na wasiwasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.