Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-RUSHWA

Kashfa ya rushwa yaendelea kutajwa katika Fifa

Vyombo vya habari nchini Uingereza vimeripoti kuwa, Morocco ndio iliyoshinda kuandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 wala sio Afrika Kusini. Hizi ni tuhma za hivi punde za kashfa za ufisadi zinazoendelea kulikabili Shirikisho la soka duniani FIFA.

Sepp Blatter, rais wa FIFA, akitangaza jina la nchi ambayo ingeliandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, Mei 15, mwaka 2004 Zurich.
Sepp Blatter, rais wa FIFA, akitangaza jina la nchi ambayo ingeliandaa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010, Mei 15, mwaka 2004 Zurich. AFP PHOTO/KURT SCHORRER
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa Morocco iliishinda Afrika Kusini kwa zaidi ya kura mbili kwa mujibu wa siri iliyotolewa na aliyekuwa Mwanakamati mkuu wa FIFA Ismail Bhamjee.

Juma lililopita, Marekani ilidai kuwa uchunguzi wa wajajusi wa FBI umebaini kuwa serikali ya Afrika Kusini ilitoa Dola Milioni 10 kupitia aliyekuwa Naibu rais wa FIFA Jack Warner ili kupigiwa kura na kuwa wenyeji wa kombe la dunia.

Hata hivyo, Waziri wa michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula alijitokeza na kukanusha madai hayo na kusema fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuendeleza na kusaidia soka katika mataifa ya Carrebian.

Bhamjee amenukuliwa akisema baada ya kuhojiwa na mwahabari mmoja kuwa, licha ya Morocco kushinda nayo pia ilitoa rushwa ya Dola Milioni 1 kwa kiogozi wa CONCACAF Jack Warner ili kupigiwa kura.

Sakata hili la FIFA limesababisha Joseph Blatter kutangaza kuwa anajiuzulu na anatarajiwa kuitisha mkutano mkuu ili kufanyika kwa uchaguzi mwingine, mwishoni mwa mwaka huu au mwanzoni mwa mwaka ujao.

Jack Warner aliyeondoka katika uongozi wa FIFA miaka minne iliyopita, juma lililopita alidokeza kuwa atatoa siri ambazo amekuwa akizihifadhi kuhusu kashfa ya ufisadi katika Shirikisho hilo la soka duniani.

Sakata hili la rushwa pia limesababisha kuwepo kwa dukuduku kuhusu usafi wa Urusi kupewa nafasi ya wenyeji wa kombe la duniani mwaka 2018 pamoja na Qatar mwaka 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.