Waasi wa MNLA wako mbioni kusitisha vita
Muungano wa makundi ya wapiganaji wa kituareg nchini Mali , unatarajiwa kusaini makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo, leo alhamisi, wapatanishi katika mgogoro unaolikumba eneo hilo, wamethibitisha.
Imechapishwa:
Mwaka wa 2013 Waasi hao wa Tuareg nchini Mali, walitangaza kusitisha harakati zao za kijeshi nchini humo.
Kulingana na taarifa kwenye mtandao wa waasi hao , kundi hilo la ukombozi wa eneo la Azawad, (MNLA) liliteka maeneo ya kutosha kuweza kuunda jimbo lao wenyewe.
Lakini kundi la wapiganaji wa kiisilamu waliosaidiana na waasi wa Tuaraeg kupigania maeneo hayo, halijatoa msimamo wake kuhusiana na mpango huu wa amani.