Pata taarifa kuu
MALI-MAPIGANO-USALAMA

Mapigano kati ya makundi ya waasi Kaskazini mwa Mali

Mapigano kati ya makundi ya waasi na wanamgambo wenye uhusiano wa karibu na serikali ya Mali yamesababisha vifo vya watu zaidi ya ishirini Alhamisi wiki hii. Mji wa Léré ulishambuliwa na kudhibitiwa na waasi Jumatano Aprili 29 na baadae kudhibitiwa na jeshi.

Mji wa Léré ambao ulishambuliwa Jumatano Aprili 29 mwaka 2015 na waasi lakini muda mchache baadae jeshi liliuweka mji huo kwenye himaya yake Alhamisi Aprili 30.
Mji wa Léré ambao ulishambuliwa Jumatano Aprili 29 mwaka 2015 na waasi lakini muda mchache baadae jeshi liliuweka mji huo kwenye himaya yake Alhamisi Aprili 30. AFP/PHOTO ERIC FEFERBERG
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa makundi ya waasi wamebaini kwamba watabaki pembezoni ya mji, na baada ya shambulio lililosababisha maafa katika mji wa Goundam, waliudhibiti Alhamisi wiki hii mji wa Bintagoungou, katika jimbo la Tombouctou. Mapigano yameendelea kushuhudiwa karibu na Ménaka.

" Hatutaki kushikilia wilaya mpya, mashambulizi yetu ni ya kutoa ulinzi sehemu tulizodhibiti baada ya kuudhibiti mji wa Menaka", mesmaji wa makundi ya waasi.

Kijiji hiki cha jimbo la Gao kilikuwa chini ya udhibiti wa vikundi vya waasi hadi Jumatatu wiki hii wakati wanamgambo wenye uhusiano na serikali ya Mali, Gatia, walipojaribu kuudhibiti mji huo.

Timu ya Upatanishi wa kimataifa imeanza majadiliano na vyama viwili kuhusu suala la Menaka ili kukomesha mapigano. Kudhibitiwa kwa kijiji hicho na makundi yenye uhusiano na serikali ni ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji mapigano. Timu ya wapatanishi imewataka wanamgambo kuondoka katika mji huo. Na huo ndio msimamo rasmi wa serikali ya Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.