Pata taarifa kuu
GUINEA-UPINZANI-MAANDAMANO-SIASA-USALAMA

Guinea : upinzani watoa wito wa kusitisha maandamano

Upinzani umesitisha maandamano yake tangu Jumanne wiki hii hadi Jumatatu ya wiki ijayo katika mji mkuu wa Guinea, Conakry. Utawala umeonyesha nia yake ya kuketi kwenye meza ya mazungumo na upinzani katika hali ya kutafutia ufumbuzi madai ya upinzani.

Kiongozi wa upinzani Guinea, Cellou Dalein Diallo ( katikati ya waandamanaji) mjini Conakry, Aprili 14 mwaka 2015.
Kiongozi wa upinzani Guinea, Cellou Dalein Diallo ( katikati ya waandamanaji) mjini Conakry, Aprili 14 mwaka 2015. AFP PHOTO / CELLOU BINANI
Matangazo ya kibiashara

Uamzi huu wa upinzani wa kusitisha kwa muda maandamano unakuja baada ya siku mbili ya machafuko katika mji wa Conakry, ambayo yalisababisha vifo vya watu wawili na watu wengi kujeruhiwa.

Upinzani unapinga dhidi ya kuahirishwa upya kwa uchaguzi wa serikali za mitaa ambao umepangwa kufanyika mwezi Machi mwaka 2016, baada ya uchaguzi wa urais utakaofanyika mwezi Oktoba ujao.

Hata hivyo makabiliano yalitokea Jumanne wiki hii kati ya waandamanaji na polisi kwenye barabara kuu ya Le Prince mjini Conakry. Askari polisi wengi waliingia mitaani, huku baadhi ya watu wakikamatwa. Wakati huohuo milio ya risasi ilisikika katika kitongoji cha Cosa mjini Conakry. Lakini Jumanne jioni upinzani ulitoa tangazo la kusitisha maandamano hayo hadi Jumatatu juma lijalo.

" Haikua suala la kufanya maandamano kila siku. Inachosha, na kila mtu ana majukumu yake nyumbani. Polisi kwa upande wake imekua ikihusika na vurugu pamoja na ukiukaji wa haki za binadamu. Na pia katika nchi hii watu wanaishi kwa kazi wanazofanya kila siku, hususan biashara kwa kuweza kupata ruzuku ya kuwawezesha kuishi", amesema Aboubacar Sylla, msemaji wa upinzani.

Maandamano yanatazamiwa kufanyika tena nchi nzima Jumatatu ijayo. Waziri mkuu wa Guinea amekutana na timu ndogo ya maafisa waandamizi serikalini na kutoa muda wa saa 24 kwa timu yake ili kutoa mapendekezo kwa lengo kuanzisha mazungumzo.

Kabla ya kushiriki katika mazungumzo ya aina yoyote na serikali, upinzani umeomba kalenda mya ya uchaguzi ifutwe pamoja na kusitishwa kwa shughuli za Tume ya uchaguzi. Utawala kwa upande wake, umeomba kusiwepo na masharti yoyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.