Pata taarifa kuu
GUINEA-SIASA-USALAMA

Guinea: Upinzani watoa wito kwa wafuasi wake wa kususia kazi

Upinzani nchini Guinea umetoa wito kwa wafuasi wake kususia kazi kwa siku nzima ya Alhamisi wiki hii, hususan katika mji mkuu wa nchi hiyo, Conakry.

Vyama saba vya kisiasa vya upinzani vimetolea wito wafuasi wao kusalia nyumbani Alhamisi Aprili 2 mwaka 2015.
Vyama saba vya kisiasa vya upinzani vimetolea wito wafuasi wao kusalia nyumbani Alhamisi Aprili 2 mwaka 2015. CC/Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza upinzani kupinga hatua dhidi ya uamuzi wa Tume ya Uchaguzi ya kubadili utaratibu wa uchaguzi, na dhidi ya kutotia katika vitendo makubaliano ya kisiasa ya mwezi Julai 2013.

Kwa jumla vyama saba vya kisiasa ambavyo vina wabunge 49 kwa jumla ya 114 katika Bunge la Guinea vimewatolea wito wafuasi wao kusalia nyumbani.

Awali upinzani ilitaka kuandaa maandamano, lakini serikali ilitangaza dharura ya afya katika mji wa Conakry na katika maeneo tisa ya Guinea, ambayo inazuia mikusanyiko.

Kutokana na dharura ya afya ambayo inawazuia wafuasi wa upinzani kuingia mitaani katika mji wa Conakry, upinzani umeamua kutoa wito kwa wafuasi wake kusalia nyumbani. Vyama saba, ikiwa ni pamoja na vyama vikuu vitatu, UFDG, UFR na PEDN, vimewatolea wito wafuasi wao kusalia nyumbani Alhamisi wiki hii kwa lengo la kuzorotesha shughuli katika mji mkuu.

Siku hii ya kuitikia wito wa kususia kazi kwa wafuasi wa upinzani ni ya kwanza ya mfululizo wa vitendo ambavyo vinatazamiwa kupanuliwa hivi karibuni kwa nchi nzima. Upinzani unaomba mabadiliko ya kalenda ya uchaguzi, ambayo imepanga uchaguzi wa urais kufanyika Oktoba 11.

Upinzani umeomba pia marekebisho makubwa ya Tume ya Uchaguzi na utekelezaji wa makubaliano ya kisiasa ya mwezi Julai 2013. Masharti matatu yamewekwa kwa ajili ya kuanza kwa mazungumzo yaliopendekezwa na serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.