Pata taarifa kuu
NIGERIA

Uchaguzi wa Magavana unaendelea nchini Nigeria

Wananchi wa Nigeria wanapiga kura kuwachagua Magavana, wiki mbili baada ya kumalizika kwa Uchaguzi wa urais.

Upigaji kura mjini Lagos
Upigaji kura mjini Lagos REUTERS/Kunle Ajayi
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huu unafanyika katika majimbo 29 kati ya 36, huku majimbo yanayosalia yakitarajiwa kushiriki katika zoezi hili baadaye.

Chama cha PDP cha rais Goodluck Jonathan anayeondoka madarakani kimekuwa na Magavana 21 dhidi ya upinzani ambao umekuwa na viti 14.

Wachambuzi wa siasa wanasema huenda chama cha upinzani APC kikafanya vizuri kwa sababu ya mgombea wake Muhamadu Buhari kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais.

Macho na masikio yapo katika mji tajiri wa Lagos, na ushindani ni mkali kati ya Akinwunmi Ambode wa chama cha APC na Jimi Agbaje wa PDP.

Jimbo la Lagos kwa kipindi kirefu limekuwa likiongozwa na upinzani, na jimbo lingine linaloangaziwa kwa makini ni lile la Rivers lenye utajiri wa mafuta pamoja na Kano lenye idadi kubwa ya watu.

Hali ya wasiwasi inashuhudiwa katika jimbo la Rivers kati ya Gavana wa sasa wa Jimbo hilo kutoka chama cha upinzani na rais Goodluck Jonathan kwa madai kuwa kura za urais ziliibiwa.

Hata hivyo, msemaji wa tume ya Uchaguzi katika jimbo hilo Tonia Nwobi, amesema kuwa mipango kabambe imewekwa kuhakikisha kile kilichotokea wakati wa Uchaguzi wa urais hakirejelewi tena .
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.