Pata taarifa kuu
NIGERIA-INEC-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Nigeria : Muhammadu Buhari aongoza Kaskazini

Matokeo ya uchaguzi yanaendelea kusubiriwa baada ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa wiki hii nchini Nigeria. Siku ya Jumatatu, Tume ya Uchaguzi ilianza kutangaza matokeo.

Afisa waliosimamia uchaguzi wamekusanyika katika ukumbi wa Port harcourt kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais katika jimbo la Rivers, Machi 30 mwaka 2015.
Afisa waliosimamia uchaguzi wamekusanyika katika ukumbi wa Port harcourt kwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais katika jimbo la Rivers, Machi 30 mwaka 2015. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya uchaguzi katika majimbo 19 kati ya 36 yalitangazwa. Licha ya mazingira ya usalama kuwa tete, uchaguzi ulifanyika kwa amani. Wanigeria na jumuiya ya kimataifa wanafuatilia kwa karibu uchaguzi huo.

Kwa sasa, bado haitoshi kujua mgombea au chama ambacho kimeshinda dhidi ya vingine. Kila mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi ya kila jimbo amekua akitangaza hadharani matokeo ya uchaguzi wa Maseneta, wa Wabunge na uchaguzi wa urais. Wajumbe hawa wamekua wakieleza jinsi uchaguzi ulivyofanyika katika maeneo waliyokua wakisimamia uchaguzi huo mkuu.

Kulingana na kura zilizohesabiwa, matokeo ya mwanzo yanaonesha kuwa muungano wa vyama vya upinzani (APC) unaoongozwa na Mahammadu Buhari, umepata kura nyingi kaskazini mwa Nigeria. Buhari ni mzaliwa wa jimbo la Katsina, ambapo chama chake kinaongoza dhidi ya vyama vingine, kikiwa na kura milioni 1.3

APC inaongoza pia katika Adamawa, katika majimbo ya Kano, Kaduna na Jigawa. Kungineko, APC inaongoza katika majimbo mengine sita. Kwa jumla muungano wa vyama vya upinzani (APC) unaongoza katika majimbo kumi.

Kwa upande wake, Goodluck Jonathan na chama chake cha PDP, wanaongoza katika majimbo saba, ikiwa ni pamoja na Ekiti, Abia, Anamba, Nasarawa na Enugu ( kusini mwa nchi), ambapo PDP imepata kura 14,157.

Lakini sasa matokeo rasmi yameanza kutangazwa, huku kukianza kujitikeza malalamiko. Katika jimbo la Rivers, machafuko yaliripotiwa siku ya uchaguzi. Katika jimbo hilo viongozi wa vyama vya upinzani wamebaini kwa uchaguzi uligubikwa na wizi, huku wakiomba matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo yafutwe. Hata hivyo serikali imechukua uamzi wa kuweka marufuku ya kutotoka nje usiku katika jimbo hilo la Rivers.

Hayo yakijiri, akiwa katika mazungunzo kuhusu mpango wa Nyuklia wa Iran katika mji wa Lausanne, waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ameelezea wasiwasi wake juu ya wizi uliyogubika uchaguzi huo.

Hata hivyo Umoja wa Afrika na Tume ya Uchaguzi nchini Nigeria wamesema wameridhishwa na uchaguzi, huku wakifutilia mbali kasoro ziliyelezwa na Marekani pamoja na Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.