Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA

Wabunge kadhaa wa upinzani wafukuzwa

Upinzani umepata pigo kubwa, baada ya wabunge ishirini na mmoja wa chama kikuu cha upinzani cha MDC kufukuzwa bungeni.

Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC.
Morgan Tsvangirai wa chama cha MDC. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Spika wa Bunge amebaini kwamba, wabunge hao si wafuasi wa chama cha MDC cha Morgan Tsvangirai.

Wabunge hao 21 walitofautiana na Morgan Tsvangirai na baadae kuunda tawi lingine la chama hicho.

Tawi hilo la chama cha MDC liliundwa na Tendai Biti mwaka mmoja uliopita, na kubaini kwamba limejitenga na Morgan Tsvangirai.

Spika wa Bunge amesema kwamba wabunge hao hawawakilishi tena chama, ambacho kiliwapa nafasi ya kupigiwa kura, na kuamua kuwafukuza. Uamzi huo unaonekana kuudhoofisha upinzani. Nafasi za wabunge hao zitachukuliwa na wabunge wengine ambao watapigiwa kura. Kutokana na mgawanyiko ambao unaripotiwa katika kambi ya upinzani, nafasi hizi huenda zikachukuliwa na chama tawala cha Zanu-PF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.