Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-Upinzani

Mgawanyiko wajitokeza katika chama cha upinzani cha MDC nchini Zimbabwe

Vuguvugu la mgawanyiko wa kisiasa ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement For Democratic Change MDC limeendelea kushuhudiwa ambapo hapo jana wafuasi wa chama hicho kwenye eneo la Mutare waliingilia kati mkutano wa kiongozi wa chama hicho, Morgan Tsvangirai wakitaka kujiuzulu kwa katibu mkuu wa chama hicho, Tendai Biti na viongozi wengine.

Picha ya zamani ya kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai akisawasabahi wafuasi wake katika uwanja wa Bulawayo.
Picha ya zamani ya kiongozi wa chama cha upinzani cha MDC, nchini Zimbabwe, Morgan Tsvangirai akisawasabahi wafuasi wake katika uwanja wa Bulawayo. RFI
Matangazo ya kibiashara

Katibu mkuu Biti na viongozi wengine wa chama hicho akiwemo naibu mweka hazima wa chama, Elton Mangoma, aliyesimamishwa na chama, wanatuhumiwa kuhusika na kupanga njama za kutaka kumpindua Tsvangirai kama kiongozi wa chama.

Toka kusimamishwa kwa Mangoma, na hatua ya Tendai Biti kutaka Morgan Tsvangirai kutoruhusiwa kuingia kwenye kikao cha mkutano wa kamati kuu ya chama kumetafisiriwa na wanachama wa MDC-T kama njama za mapoinduzi dhidi ya kiongozi wao.

Viongozi hao wanataka Tsvangirai asipewe nafasi nyingine ya kuwania kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Mvutano huo ulianza kushuhudiwa toka mwanzoni mwa mwezi wa machi punde tu baada ya tangazo la kamati ya utendaji kutangaza kumsimamisha kwa muda naibu muweka hazina Elton mangoma kufuatia matamshi yake ya kumtaka kiongozi wa chama hicho kuachia ngazi.

Lakini katika kile kinachoonekana kuwa bado kuna mgawanyiko ndani ya chama hicho hata katibu mkuu wake Tendai Biti anaonekana kutofautiana na mwenyekiti wake kuhusu kuruhusiwa kushiriki wakati wa mkutano wa kamati kuu ya chama.

Wachambuzi wa mambo wameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa tofauti ndani ya chama hicho na kwamba kunatoa mwanya kwa chama tawala cha ZANU-PF kuendelea kujipatia umaarufu.

Hofu ya kushuhudiwa mgawanyiko zaidi ndani ya chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for democratic Change MDC, imeendelea kutanda wakati huu ambapo uongozi wa chama hicho ukiwataka viongozi waliochoka kuwemo ndani ya chama hicho kujiondoa wenyewe.

Msimamo wa chama hicho umetolewa mwanzoni mwa mwezi wa machi na rais wake, Morgan Tsvangirai ambaye ameendelea kusisitiza kuwa hatoondoka madarakni kwa shinikizo la viongozi wachache wenye kutaka kumpindua.

Kauli ya Tsvangirai aliitoa ikiwa zimepita siku mbili tu, toka chama hicho kitangaze kumsimamisha kwa muda naibu mweka hazina wa chama hicho, Elton Mangoma kufuatia matamshi yake ya hivi karibu kumtaka kiongozi huyo kujiuzulu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.