Pata taarifa kuu
TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Tunisia : watu tisa wakamatwa baada ya shambulio

Hali ya taharuki imeendelea kutanda katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis, baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kuwateka nyara watalii na wengine kuuawa katika makavazi ya Bardo jijini Tunis Jumatano wiki hii.

Shambulio katika makavazi ya Bardo katika mji mkuu wa Tunisaia, Tunis, yamezimwa baada ya operesheni ya vikosi vya usalama,  tarehe 18 Machi mwaka 2015.
Shambulio katika makavazi ya Bardo katika mji mkuu wa Tunisaia, Tunis, yamezimwa baada ya operesheni ya vikosi vya usalama, tarehe 18 Machi mwaka 2015. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Watu ishirini na mmoja wengi wao wakiwa watalii waliuawa. Uchunguzi umeanzishwa, na washukiwa tisa wamekamatwa Alhamisi wiki hii, kwa mujibu wa Ikulu ya Tunis. Watu hao wanasadikiwa kuwa walikua wakiwasiliana na wauaji hao walioendesha shambulio katika makavazi ya Bardo.

Shambulio hilo lilitokea Jumatano wiki hii katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis. Vyanzo vya usalama vya Tunisia vimebaini kwamba vijana wenye umri wa miaka zaidi ya ishirini waliingia katika makavazi ya Bardo na kuanza kufyatulia risasi basi saba ziliyokuemo watalii, ambazo zilikua ziliegesha sehemu hio. Kwa mujibu wa mashahidi ambao wameongea na RFI Alhamisi asubuhi wiki hii, baadhi ya watalii waliuawa kwa risasi ziliyokua zikifyatuliwa hovyo.

Vijana hao wawili, mmoja kutoka mji wa Kasserine na mwengine kutoka kata moja ya mji wa Tunis, karibu na kata ya Bardo, waliingia na mateka katika makavazi ya Bardo, na sehemu hio ndipo waliuawa na vikosi vya usalama vya Tunisia. Haijajulikana iwapo vijana hao ni kutoka tawi la kundi la Aqmi la Okba Ibn Nafaâ linaloendesha harakati zake tangu mwaka 2012  kwenye mpaka wa Algeria, au ni kutoka kundi la wapiganaji wa Dola la Kiislamu ambalo linaendesha harakati zake Syria, Iraq au nchini Libya.

Inaaminika kuwa raia wengi wa Tunisia wamejiunga na makundi ya kijihadi katika nchi mbalimbali. Takriban raia wa Tunisia, kwa mujibu wa takwimu rasmi, wanapigana kwa sasa nchini Syria na Iraq. 500 miongoni mwa raia hao wamerejea Tunisia, kwa mujibu pia wa takwimu rasmi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.