Pata taarifa kuu
TUNISIA-Uchaguzi-Siasa

Beji Caid Essebsi amekuwa rais rasmi Tunisia

Tunisia imekua sasa na rais mpya, ambaye ni wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia. Beji Caid Essebsi, mwenye umri wa miaka 88, ameapishwa hii Jumatano Desemba 31 mwaka 2014 asubuhi, kabla ya kuendelea na sherehe zingine za kiitifaki.

Rais Beji Caid Essebsi, muda mfupi kabla ya kuapishwa mbele ya Bunge tarehe 31 Desemba mwaka 2014.
Rais Beji Caid Essebsi, muda mfupi kabla ya kuapishwa mbele ya Bunge tarehe 31 Desemba mwaka 2014. REUTERS/Zoubeir Souissi
Matangazo ya kibiashara

Beji Caid Essebsi amejielekeza leo Jumatano mchana katika jengo la Carthage ambalo ni makao makuu ya Ikulu, kwa minajili ya kukabidhiana madaraka na aliye kua mshindani mwenzake, Moncef Marzouki, ambaye alishindwa katika uchaguzi wa urais.

Muda mfupi kabla, kwenye majira ya asubuhi, ilikuwa ni sherehe za kuapishwa kwa rais, sherehe ambayo imefanyika ndani ya jengo la Bunge la Tunisia.

" Naapa kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu kuwa ntahifadhi uhuru wa Tunisia na kuheshimu mipaka ya nchi, kuheshimu Katiba na sheria." Kwa maneno hayo, Beji Caid Essebsi, mwenye umri wa miaka 88, amekuwa rais mpya wa Tunisia. Beji Caid Essebsi ni rais wa kwanza kihistoria, ambaye alichaguliwa kirahisi katika uchaguzi wa moja kwa moja ambao raia walitakiwa kupiga kura.

"Hakuna maendeleo ya baadaye kwa nchi ya Tunisia iwapo hakutokua na makubaliano kati ya vyama vya siasa", amesema pia rais mpya. Pengine akimaanisha mazungumzo yanayoendelea kwa kuunda serikali mpya. ECB, ambaye chama chake cha Nida Tounes hakikupata idadi inayohitajika ya Wabunge, kitalazimika kufanya muungano na vyama vingine ili kiweze kupata idadi Wabunge wengi.

Jumatano Desemba 31 mwaka 2014 alasiri, Waziri mkuu wa sasa Mehdi Joma, amewasilisha barua ya kujiuzulu, lakini timu yake itaendelea kusimamia mambo muhimu mpaka Januari 14, siku ya maadhimisho ya mapinduzi. Siku moja ambayo imechaguliwa kwa ajili ya sherehe kubwa ya kutawazwa kwa BCE, mbele ya marais kadhaa kutoka mataifa ya kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.