Pata taarifa kuu
UKRAINE

UNSC yatazamiwa kukutana kwa dharura kuhusu Ukraine

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataraji kukutana kwa dharura kesho Jumapili ili kuweka mikakati ya kuimarisha makubaliano ya kusitisha mapigano Mashariki mwa Ukraine yaliyofikiwa mjini Minsk nchini Belarus, wanadiplomasia wamesema.

Ukrainian President Petro Poroshenko( mbele) akiondoka baada ya mazungumzo ya kusaka amani mashariki mwa Ukraine.
Ukrainian President Petro Poroshenko( mbele) akiondoka baada ya mazungumzo ya kusaka amani mashariki mwa Ukraine. Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Wajumbe 15 wa baraza hilo wanajiandaa kupitisha mapendekezo yaliyoandaliwa na Urusi yanayotoa wito kwa pande zote kutekeleza makubaliano hayo ambayo yanatoa makataa ya kusitisha vita kuanzia kesho Jumapili.

Makubaliano yaliyofikiwa na rais wa Urusi Vladimir Putin na viongozi wa Ukraine , Ufaransa na Ujerumani, yameonekana kushindwa huku mapigano makali ya jana Ijumaa yakisababisha vifo vya watu 28.

Mapigano hayo kati ya jeshi la Ukraine na waasi wanaoiunga mkono serikali ya Urusi yanalenga kuudhibiti mji wa Debaltseve, mji unaolezwa kuwa muhimu kwa wapiganaji hao

Mkataba wa amani ulioafikiwa kati ya Ukraine na Urusi, chini ya wasuluhishi Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais wa Ufaransa Francois Hollande unatarajiwa kuanza kutekelezwa leo usiku.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.