Pata taarifa kuu
DRC-M23-KENYA-UGANDA-WAKIMBIZI-MAKUBALIANO

Wapiganaji wa zamani wa M23 warejeshwa DRC

Kundi la waasi wa zamani wa M23 limelani Jumanne Desemba 16, zoezi la kuwarejesha makwao kwa nguvu lililofanywa na jeshi la Uganda katika kambi ya jeshi ya Bihanga, kwenye umbali wa kilomita 300 kusini magharibi mwa Kampala.

wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014.
wapiganaji wa kundi la zamani la M23, Februari 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wa zamani wa M23 walikua wakipewa hifadhi katika kambi hii ya kijeshi. Kwa mujibu wa kiongozi wa M23, Bertrand Bisimwa, wakati wa operesheni hiyo, wapiganaji kadhaa wa kundi la zamani la waasi la M23 walijeruhiwa na mmoja alifariki.

“ Ni pigo kubwa kwa serikali ya Kinshasa, ambayo imekiuka makubaliano yaliyoafikiwa Nairobi, kwa kulazimisha turejeshwe kwa nguvu. Mapema leo asubuhi wamewasili wakiwa na magari ili warejeshe kwa nguvu wapiganaji wetu", amesema Bisimwa.

" Hata hivyo wanajeshi wetu hawakukubaliana na zoezi hilo. Baadae jeshi la Uganda lilitumia nguvu na kuwajeruhi wapiganaji kadhaa. Tuna taarifa kwamba kuna wapiganaji ambao wamefariki, huku baadhi ya wapiganaji wetu wakiamua kutoroka kambi kambi hiyo”, ameongeza Bertrand Bisimwa.

Kwa upande wake, msemaji wa jeshi la Uganada, Paddy Ankunda, akihojiwa na RFI, amekanusha kuwa jeshi la Uganda limetumia nguvu zaidi katika zoezi hilo, huku akibaini kwamba wapiganaji wazamani wa M23 walitoroka kambi waliyo kuwemo wakati walipoona magari ambayo yalikua yameletwa kuwasafirisha hadi Congo.

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Uganda, Paddy Ankunda, wapiganaji 120 kati ya 330 ambao wamepewa msamaha na serikali ya Congo wamekubali kurejea kwa hiari yao na wengi miongoni mwao wako njiani wakirudi Congo. Msemaji wa jeshi la Uganda, amebaini kwamba maelfu ya wapiganaji hao wa zamani wa M23 walifaulu kutoroka, lakini polisi imeanza kuwatafuta, amesema Paddy Ankunda,

Wakati huohuo, serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lambert Mendé ameonya dhidi ya taarifa za uongo zinazoendelea kutolewa na M23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.