Pata taarifa kuu
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-Msamaha

Waasi wa zamani wa kundi la M23 wamepewa msamaha na rais Joseph Kabila.

Rais wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila ametangaza msamaha kwa waasi wa zamani wa kundi la M23 ambao walishindwa katika vita na majeshi ya DRC na Umoja wa Mataifa. Msamaha huo utahusisha makosa ya uasi, vita na makosa mengine ya kisiasa yaliyofanywa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo mpaka kufikia Disemba 20 mwaka 2013 siku ambayo serikali ya Kabila iliidhinisha muswada huo wa msamaha.

Rais wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange
Rais wa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila Kabange RFI
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia hatua hiyo waasi wa zamani wa M23 wana miezi sita ya kuwasiliana na serikali ili waweke ahadi ya kimaandishi wakieleza kuwa kamwe hawatarejea tena katika uasi.

Umoja wa Mataifa ukifuatiwa na nchi za magaharibi umeunga mkono tamko hilo la rais Kabila na kusema kuwa hiyo inatoa fursa ya DRC kufungua ukurasa mpya baada ya kufanyika uasi mashariki mwa nchi hiyo.

Hata hivyo wanaharakati na Mashirika ya kiraia yanapinga hatua hiyo kwa madai kuwa uasi uliofanyika ulidhulumu haki za raia kwa kutekeleza mauaji na vitendo ya ubakaji.

Wakati huohuo Umoja wa Ulaya nchini DRCongo umeendelea kutetea kauli yake ya kuitaka serikali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kuheshimu sheria ya upinzani kwa kuwapa haki ya kujitetea wapinzani.

Kauli ambayo ilitolewa mwanzoni mwa juma hili na Ujumbe wa Umoja wa ulaya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufutia hatuwa ya kuzuiliwa kwa mwanasiasa wa upinzani Vital Kamerhe kusafiri kuelekea mjini Goma.

Koene Vanvaeke, ambaye ni mjumbe wa EU amesame wakati nchi hiyo ikielekea kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2016, uhuru wa kutowa maoni ni swala muhimu na kupata maoni tofauti ndio kukuwa kwa demokrasia.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.