Pata taarifa kuu
LIBERIA-GUINEA-SIERRA LEONE-COTE D'IVOIRE-WHO-Afya-Siasa

Ebola: mkutano wa kilele Afrika ya Magharibi

Mkutano wa kikanda kuhu virusi vya Ebola unafanyika ijumaa wiki hii katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, ambapo watahudhuria marais wa Guinea, Liberia,Sierra Leone na Côte d'Ivoire. Watu 700 wameuawa baada ya kuambukizwa virusi hivyo vya Ebola katika baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi.

Mkutano wa kikanda kuhusu jinsi ya kupambana na virusi vya Ebola unaanza nchini Guinea.
Mkutano wa kikanda kuhusu jinsi ya kupambana na virusi vya Ebola unaanza nchini Guinea. REUTERS/Samaritan's Purse/Handout via Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sierra Leone na Liberia zimechukua hatua kali za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola, ambao unaendelea kuenea katika katika mataifa jirani ya nchi hizo. Shirika la afya duniani WHO limetoa kitita cha dola milioni 100 kwa kupambana na ugonjwa wa Ebola.

Mkurugenzi wa shirika la afya duniani, Margaret Chan, atahudhuria mkutano huo wa Conakry kwa kuanzisha mpango wa WHO wa kupambana na Ebola.

Chan amesema kwamba Who inatiwa hofu na virusi vya Ebola, abavyo vinaendelea kusika kasi katika mataifa ya Afrika, na vimesababisha vifo vya watu 729 ( 339 nchini Guinea, 233 Sierra Leone na 156 Liberia) kulingana na idadi iliyotolewa alhamisi wiki hii na shirika la afya duniani.

Chan ameongeza kuwa mpango huo wa kitita cha dola 100 unalenga kuwapa ajira wafanyakazi zaidi ya 100 watakaojihusisha na masuala ya kiutu ili kuimarisha jitihada za WHO kwa kupambana na Virusi vya Ebola ambavyo vinaendelea kushika kasi barani Afrika.

Wakati huo huo mkurugenzi wa vituo vya ukaguzi na kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya maambukizi nchini Marekani, Tom Frieden, ametangaza kuwatuma wataalam 50 Afrika Magharibi mnamo siku 30 zijazo, akibaini kwamba watahakikisha mnamo miezi mitatu kuwa ugonjwa huo umetokomezwa.

Mataifa ya Afrika Magharibi yajipanga kukabiliana na virusi vya Ebola.
Mataifa ya Afrika Magharibi yajipanga kukabiliana na virusi vya Ebola. REUTERS/Samaritan's Purse

Hata hivo hatua za kukabiliana na virusi vya Ebola zinaendea kuchukuliwa barani Afrika hata kungineko ulimwenguni.

Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, wametangaza kwamba wameanzisha mikakati mipya ya kupambana na Ebola.

Virusi vya Ebola havina kinga, na ishara za ugonjwa huo ni kutapika, kuharisha na kutokwa na damu kinywani, puani na sehemu zingine za siri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.