Pata taarifa kuu
RWANDA-FDLR-CNR-Siasa-Sheria

Rwanda : luteni Joël Mutabazi akabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha

Ofisi ya mashtaka nchini Rwanda imeomba mahakama kutoa adhabu ya kifungo cha maisha dhidi ya afisa wa zamani wa jeshi luteni Joël Mutabazi, aliekua katika kikosi cha ulinzi wa rais.

Kesi ya Joël Mutabazi kushoto) na watuhumiwa wenzake imeanza kusikilizwa mjini Kigali, nchini Rwanda.
Kesi ya Joël Mutabazi kushoto) na watuhumiwa wenzake imeanza kusikilizwa mjini Kigali, nchini Rwanda. AFP PHOTO/ Stéphanie Aglietti
Matangazo ya kibiashara

Mutabazi na watuhumiwa wenzake, kwa mujibu wa ofisi ya mashtaka, wanahusishwa katika uhalifu mbalimbali wa mashambulizi kwa gruneti yaliyopelekea usalama kudorora mjini Kigali mwaka 2010.

Msahambulizi hayo yalihusishwa waasi wa kihutu wa Rwanda wa FDLR kwa ushirikiano na chama cha upinzani kiliyoko nje ya nchi cha RNC.

Joël Mutabazi (katikati) anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela.
Joël Mutabazi (katikati) anakabiliwa na adhabu ya kifungo cha maisha jela. AFP PHOTO/ Stéphanie Aglietti

Luteni Joël Mutabazi, alihukumiwa tangu Januari 28 na mahakama ya kijeshi kwa makosa 6 : “ uanzilishi wa kundi la watu wenye silaha”, “ kupanga njama dhidi ya rais”, “ ugaidi”, “ kupanga njama dhidi ya serikali iliyoteuliwa”, “ kumiliki silaha kinyume cha sheria” na “ utoro katika jeshi”.

Kulingana na tuhuma hizo, ofisi ya mashtaka imeomba mahakama kutoa adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya luteni Joël Mutabazi, na kuiomba imuondowe kwenye orodha ya wanajeshi wa Rwanda.

Ofisi ya mashtaka imeomba pia adhabu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya mtuhumiwa mwenzake, Joseph Nhimiyimana, ambaye inamtuhumu kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa kwa kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda FDLR na RCN, Watuhumiwa wengine tisa, wameombewa adhabu ya kifungo cha miaka 37 jela, na kifungo cha miaka 20 jela ya watuhumiwa wengine wawili.

Ofisi ya mashtaka imeomba pia kifungo cha miaka kati ya 7 na 5 dhidi ya mjomba wa Joël Mutabazi, nduguye na mke wa kaka yake. Wote hao watatu walitoa ushahidi dhidi ya Joël Mutabazi.

“ Tuhuma zote hizo dhidi yangu zilitengenezwa, sina hatia na naomba niachiwe huru mara moja”amesema Joël Mutabazi, ambaye anajitetea bila hata hivo kuwa na mwanasheria, mwanasheria wake alijiondoa katika kesi hiyo, akibaini kwamba mteja wake haheshimu utaratibu wa jinsi anavyomtetea

Joël Mutabazi alikamatwa nchini Uganda na kutumwa nchini Rwanda, baada ya shirika linalohudumia wakimbizi kulani HCR kulani jinsi alivyokamatwa, wakati alikua ni mkimbi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.