Pata taarifa kuu
RWANDA-FDLR-Sheria-Usalama

Waasi wa Kihutu wa Rwanda walani kukamatwa kwa baadhi ya watu nchini Rwanda

Kundi la waasi wa kihutu wa Rwanda wanaopiga kambi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo FDLR wamelaani vikali hatuwa ya kukamatwa kwa watu wanaoshukiwa kupanga njama za kuyumbisha usalama wa Kigali ambao walikamatwa hivi karibuni.

Wapiganaji wa kundi la waasi wa kihutu la FDLR, katika moja ya misitu ilioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwaka 2009.
Wapiganaji wa kundi la waasi wa kihutu la FDLR, katika moja ya misitu ilioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mwaka 2009. REUTERS/Finbarr O"Reilly
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliotolewa na kanali Willy Irategeka kaimu katibu mtendaji wa kundi la wapiganaji Abacunguzi, amesema serikali ya Rwanda imewatia nguvuni wale wote ambao hawataki kuungana na mpango wake uliokinyume kabisa na demokrasia.

“Serikali ya Rwanda imeamua kuwakamata mwanamuziki Kizito Mihigo, mwanahabari Cassien Ntamuhanga na mwanajeshi alierejeshwa katika maisha ya kiraia Jean Paul Dukuzumuremyi, ikiwatuhumu kushirikiana na makundi ya wapinzani ya FDLR na NRC walioko ukimbizini nje ya nchi.

Hizo ni mbinu za serikali za kutaka kuwakandamiza wale wote wasiyounga mkono utawala wa Paul Kagame”, amesema kaimu katibu mtendaji wa kundi la wapiganaji la Abacunguzi (Foca),Willy Irategeka, katika tangazo liliyotolewa jumamosi iliyopita.

Polisi ya Rwanda inasema inao ushahidi wa kutosha unaonyesha watu hao watatu walikuwa wamepanga kutekeleza mashambulizi dhidi ya serikali wakishirikiana na kundi la RNC linalo husiana na Patrick Karegeya, kiongozi wa zamani wa idara ya ujasusi nchini Rwanda aliauwa mwanzoni mwa kwaka 2014 nchini Afrika Kusini.

Watu hao wanatuhumiwa pia kushirikiana na kundi la FDLR ambalo wafuasi wake wameorodheshwa katika kundi lililoshiriki katika mauaji ya kimbari yaliotekelezwa nchini Rwanda mwaka 1994.

Kizito Mihigo akiongea na waandishi wa habari mjini Kigali, aprili 15 mwaka 2014, baada ya kupata taarifa ya kukamatwa siku moja kabla.
Kizito Mihigo akiongea na waandishi wa habari mjini Kigali, aprili 15 mwaka 2014, baada ya kupata taarifa ya kukamatwa siku moja kabla. AFP PHOTO / STEPHANIE AGLIETTI

Leo hii, Kizito Mihigo na wenzake wakiwemo askari mmoja wa zamani na mwandishi wa habari wa Redio “Amazing Grace” Cassien Ntamuhanga wanatarajiwa kufikishwa mbele ya Mahakama kuu mjini Kigali kujibu mashtaka yanayowakabili.

“Maovu na ugaidi vinavyotendwa na utawala wa RPF vinapaswa kukomeshwa na kulaniwa na dunia nzima, na wale waliyokamatwa na kuziwiliwa jela wanapaswa kuachiwa huru”, limeendelea kubaini kwa lugha za kinyarwada na kingereza kundi la FDLR.

“ watu wengi walikamatwa kwa tuhuma zisiyokua na msingi za kushirikiana na kundi la FDLR”, hususan kaskazini mwa nchi, limeendelea kufahamisha tangazo hilo, huku likibaini kwamba wanyarwanda wengi wameamua kuacha makaazi yao na kukimbilia mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo kwa kuhofia usalama wao.

Mwishoni mwa mwaka wa 2013, kundi la wapiganaji la Foca lilifahamisha kwamba liko tayari kuweka silaha chini, na liliiomba jumuiya ya kimataifa kuishawishi serikali ya Rwanda kukubali kuanzisha mazungumzo na kundi hilo bila masharti, jambo ambalo lilitupiliwa na serikali ya Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.