Pata taarifa kuu
UFARANSA-RWANDA-Mauaji ya kimbari

Mjadala waibuka Ufaransa kufuatia kauli za rais Paul Kagame

Kauli za Rais Paul Kagame wa Rwanda kuhusu jukumu la Ufaransa katika kushiriki kwenye mauwaji ya kimbari nchini humo zimeibua mjadala nchini Ufaransa. Magazeti kadhaa, mashirika ya kiraia na wanasiasa wametoa wito kwa serikali kuondoa hali yoyote ya siri za nyaraka zake za mahusiano kati ya Ufaransa na Rwanda.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akilihutubia taifa kwenye uwanja wa mpira  Amohoro, mjini Kigali, aprili 7 mwaka 2014.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akilihutubia taifa kwenye uwanja wa mpira Amohoro, mjini Kigali, aprili 7 mwaka 2014. REUTERS/Noor Khamis
Matangazo ya kibiashara

Akihojiwa na RFI, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Romain Nadal , amesema kuwa kazi ya nyaraka za serikali kwa madhumuni hayo tayari imekamilishwa na tume iliyoongozwa na Paul Quiles mwaka 1998 .

“Kwa ombi la Bunge tulianza kazi ya kupekuwa nyaraka za serikali ili kubaini ukweli na katika idara zote, na takriban nyaraka elfu kumi zimekaguliwa na tume hiyo ya bunge na hadi sasa nadhani kuwa nchi ya Ufaransa ndiye nchi pekee ambayo imeruhusu nyaraka zake ziwekwe wazi na kazi hiyo imefanywa tangu mwaka 1998”, amesema Nadala.

Vyombo vya habari nchini Ubelgiji vimeelezea jana uamzi wa serikali ya Ufaransa wa kususia kushiriki katika maadhimisho ya miaka 20 ya mauwaji ya Kimbari, na kubaini kwamba Ubelgiji imefaulu kukiri makosa iliyofanya katika enzi za ukoloni.

Ujumbe wa Ufaransa uliotarajiwa kuwasili nchini Rwanda kushiriki juzi jumatatu kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ishirini tangu mauaji ya kimbari yatokee nchini humo uliamua kutoshiriki.

Hata balozi wa Ufaransa mjini Kigali, ambae alitakiwa kuliwakilisha taifa lake, hakushiriki akifahamisha kwamba hakupata kibali maalumu kinachotolewa na itifaki ya Rwanda kwa viongozi wanaohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari.
Watu 800.000 kutoka jamii ya watutsi na wahutu waliyokua wakipinga utawala wa rais Juvenal Habyarimana, waliuawa baada ya ya rais huyo kufariki katika ajali ya ndege iliyodunguliwa kwenye uwanja wa ndege wa Kanombe mjini Kigali, tarehe 6 kuamkia 7 aprili mwaka 1994.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.