Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA-Maadhimisho

Rwanda yaadhimisha miaka 20 ya mauaji ya kimbari: Ufaransa yasusia

Nchi ya Rwanda hii leo inaanza juma la maombolezo ya mauaji ya Kimbari yaliyoshuhudiwa nchini humo mwaka 1994 . Maadhimisho ya mwaka huu yanahudhuriwa na viongozi wengi zaidi kuliko ilivyowahi kushuhudiwa kwenye maadhimisho ya miaka iliyopita.

Kanisa la Ntarama, ambako watu elfu tanu kutoka jamii ya watutsi waliuawa baada ya kupewa hifadhi aprili 15 mwaka 1994.
Kanisa la Ntarama, ambako watu elfu tanu kutoka jamii ya watutsi waliuawa baada ya kupewa hifadhi aprili 15 mwaka 1994. RFI/N.C
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo ujumbe wa Ufaransa uliotarajiwa kuwasili nchini Rwanda kushiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka ishirini tangu mauaji ya kimbari yatokee nchini humo umeamua kutoshiriki. Hata balozi wa Ufaransa mjini Kigali, ambae ametakiwa kuliwakilisha taifa lake, amefahamisha kwamba hatoshiriki katika sherehe hizo, akibaini kwamba hakupata kibali maalumu kinachotolewa na itifaki ya Rwanda kwa viongozi wanaohudhuria sherehe ya maadhimisho ya miaka 20 ya mauaji ya kimbari.

Waziri wa sheria wa Ufaransa Christine Taubira alitarajiwa kuongoza ujumbe huo, lakini hatua ya kusitisha ushiriki wa nchi hiyo unatokana na matamshi ya viongozi wa Rwanda kuendelea kuituhumu Ufaransa kuhusika kwa njia moja au nyingine kwa kile kilichotokea nchini Rwanda mwaka 1994, wakati Ufaransa ilikua iliwatuma wanajeshi wake kuwalindia usalama raia katika maeneo yaliyokua yalitengwa, ambayo yalijulikana kwa jina la “zone turquoise”.

Kauli hiyo ya rais Kagame haikutofautiana na ya waziri wake wa mambo ya ndani Louise Mushikiwabo ambaye amekosoa hatua ya serikali ya Ufanaransa kusitisha ushiriki wao kwenye sherehe hizo na kusema kuwa licha ya hayo, bado historia ina nafasi yake.

Katika hatua nyingine, rais Kagame amegusia mahusiano ya nchi yake na baadhi ya nchi nyingine ikiwemo Afrika Kusini ambayo imeghadhabishwa na ushiriki wa baadhi ya wanadiplomasia wa Rwanda katika jaribio la kumuua Jenerali Faustin Kayumba Nyamwasa, na kubainisha kuwa bado nchi yake inahitaji uhusiano mzuri na Afrika kusini kwa vile bado tuhuma hizo hajizathibitishwa.

Rais Kagame ataongoza sherehe hizo kwenye uwanja wa mpira wa Amahoro, ambapo wakiwepo baadhi ya marais na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon, huku nchi ya Burundi nayo ikiazimisha kumbukumbu ya miaka ishirini ya rais wao Cyprien Ntaryamira ambaye aliuawa kwenye ndege pamoja na rais wa zamani wa Rwanda Juvenal Habyarimana.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.