Kenya: wanajeshi wawili wauawa
Nchini Kenya wanajeshi wawili wa nchi hiyo wamepoteza maisha baada ya msafara wao kushmabuliwa na watu wanaominiwa kuwa wa kundi la Kigaidi la Al Shabab katika eneo la Lamu karibu na mpaka wa nchi hizo mbili. Wakuu wa usalama nchini Kenya wamekubaliana na Mahakama kupambana na ugaidi.
Imechapishwa:
Cheza - 01:56
Hali ya usalama imekua ikidorora siku baada ya siku nchini Kenya, hususan katika miji ya Nairobi na Mombasa, miji inayo aminika kuwapa hifadhi raia wa wengi wa Somalia.
Awali Serikali ya Kenya iliwataka raia kushirikiana na vyombo vya usalama ili kukabiliana na mashambulizi ya hapa na pale ambayo yanaendelea kushuhudiwa nchini Kenya. Serikali ilibaini kwamba itahakikisha usalama umezingatiwa nchini kote.
Hivi karibuni polisi ya Kenya ilianzisha operesheni ya kupambana na makundi ya wanamgambo wa kislamu kutoka Somalia ambayo yanadaiwa kuendesha mashambulizi hayo. Polisi imekua ikiendesha msako dhidi ya raia Somalia ambao wanaendelea kuishi nchini humo kinyume cha sheria, na kuwarejesha makwao.
Kenya imekua ikishuhudia mashambulizi, baada ya kuwatuma wanajeshi wake nchini Somalia kujiunga na kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika kinachosimamia amani nchini humo.
Hivi karibuni kundi la al Shabab limetishia kuanzisha mashambulizi nchini Kenya.