Pata taarifa kuu
KENYA-NAIROBI-AFRIKA MASHARIKI

Idadi kubwa ya mateka walioshikiliwa na wanamgambo wa Al shabab waokolewa na jeshi la kenya limedhibiti jengo la Westgate

Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Joseph Ole Lenku amesema Idadi kubwa ya mateka wameokolewa na Jeshi la Kenya baada ya kudhibiti sehemu kubwa ya jengo la kibiashara Westgate katika operesheni ya kuhakikisha wanawakomboa mateka waliokuwa wakishikiliwa na wanamgambo wa kundi la Alshabab ambao walivamia na kuteka eneo hilo jumamosi mchana.

Wanajeshi wa Kenya wakiwa katika harakati za kuhakikisha ulinzi katia maeneo yote ya jengo la kibiashara la Westgate
Wanajeshi wa Kenya wakiwa katika harakati za kuhakikisha ulinzi katia maeneo yote ya jengo la kibiashara la Westgate salon.com
Matangazo ya kibiashara

Ole Lenku ameongeza kuwa mpaka sasa Idadi rasmi ya watu waliopoteza maisha imefikia 62 wakati majeruhi wakifikia 175 wakati  wapiganaji wawili wa Alshabab wamethibitika kuuawa na wengine baadhi kujeruhiwa.

Misaada ya aina mbalimbali imeendelea kutolewa ikiwemo zoezi la uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya majeruhi ambao wengine wamefanyiwa upasuaji.

Tukio la mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Al-Shabab kwenye maduka ya westgate nchini kenya limezusha hofu miongoni mwa mataifa ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi za Maziwa makuu.

Serikali za Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi zimelaani shambulio hili na kutoa pole kwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pamoja na wananchi wa taifa hilo ambao wamepoteza ndugu zao.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa kenya kwasasa inakabiliwa na changamoto kubwa ya kiusalama hali ambayo ni lazima nchi jirani ziimarishe usalama kwenye mipaka yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.