Pata taarifa kuu
SYRIA-HRW-VIKWAZO-USALAMA

Human Right Watch yaomba vikwazo dhidi ya serikali ya Syria

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) limeomba vikwazo dhidi ya waliohusika na shambulio la kemikali nchini Syria.

Wakazi wa Khan Cheikhoun wakipata huduma baada ya shambulio la kemikali lililotokea Jumanne (Aprili 4).
Wakazi wa Khan Cheikhoun wakipata huduma baada ya shambulio la kemikali lililotokea Jumanne (Aprili 4). REUTERS/Ammar Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Ombi hilo linakuja siku moja baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhitimisha kwamba serikali ya Syria ilihusika mashambulizi ya gesi aina ya sarin kwenye mji wa Khan Cheikhoun.

Shambulio la Aprili 4 katika mji huu wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Idleb yaliua watu 83, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Shirika la Haki za Binadamu nchini Syria la OSDH limetoa idadi ya watu 87 waliouawa ikiwa ni pamoja na watoto 30.

Siku ya Alhamisi, ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa na Shirika linalopiga Marufuku silaha za kemikali (OPCW) ilibaini kwamba serikali ya Syria ilihusika katika shambulio hilo, ambalo lilipelekea Marekani kuzindua mashambulizi ya kipekee dhidi ya kambi ya kikosi cha wanahewa nchini Syria.

"Baraza la Usalama linapaswa kuchukua hatua za haraka ili kuhakikisha kwamba sheria imefuatwa, na kuweka vikwazo dhidi ya watu binafsi na idara zilizohusika katika shambulio la kemikali nchini Syria," Human Right Watch, yenye makao yake New York, imesema katika taarifa yake.

Shirika hili limeomba "kukomesha udanganyifu na nadharia za uwongo zinazoenezwa na serikali ya Syria".

"Matumizi ya mara kwa mara ya Syria silaha za kemikali ni tishio kubwa kwa marufuku ya kimataifa ya matumizi ya silaha za kemikali," amesema Ole Solvang, naibu mkurugenzi wa Kitengo cha Dharura wa Human Right Watch, ambaye amesema kwamba "nchi zote zinaombwa kutuma ishara yenye nguvu kwamba uovu huu hauwezi kuvumiliwa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.