Pata taarifa kuu

Gaza: Nchi za Kiarabu kutetea UNRWA kwenye Umoja wa Mataifa

Wakuu wa diplomasia wa nchi za Kiarabu wako New York kuunga mkono Palestina kugombea kuwa mwanachama kwenye Umoja wa Mataifa (UN), lakini wameamua kutosubiri ukaguzi wa kutoegemea upande wa UNRWA na kusukuma Baraza la Usalama kukutana Jumatano. Malengo yao: kupitia upya jukumu la UNRWA, muhimu katika misaada ya kibinadamu na elimu ya Wapalestina katika maeneo yanayokaliwa - lakini pia nchini Lebanon, Jordan au Misri - na kushtumu kwa nini hasa Israel inaichukulia vibaya UNRWA.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi (kushoto) na Mwakilishi Maalum wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Ziad Abu Amr (kulia) Aprili 17, 2024 wakati wa mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi (kushoto) na Mwakilishi Maalum wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Ziad Abu Amr (kulia) Aprili 17, 2024 wakati wa mkutano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York. AFP - CHARLY TRIBALLEAU
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko New York, Carrie Nooten

Israel tayari imewashutumu wafanyakazi 450 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) kwa kuwa wanamgambo wa Hamas. Mnamo tarehe 17 Aprili, balozi wa Israel alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kwamba asilimia 17 ya wafanyakazi 13,000, au karibu watu 2,000, walikuwa na uhusiano na makundi ya kigaidi, na akatoa wito wa kuvunjwa kwa shirika hilo.

Lakini kwa upande wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan, kama Kamishna Mkuu wa UNRWA, Philippe Lazzarini, lengo kuu la Israeli ni la kisiasa zaidi. "Mashambulizi dhidi ya UNRWA hayatokani na kutoegemea upande wowote. Sababu ya haya yote ni kuwavua hadhi wakimbizi wa Kipalestina. Hiki ndicho kiko hatarini leo,” amesema Ayman Safadi.

Tangu mwaka 1948 na kuondoka kwao kutoka kwa ardhi zao, wakimbizi wa Kipalestina wamekuwa na hadhi ya kipekee duniani, ambayo inasimamiwa na UNRWA: vizazi vyao, hata kama walizaliwa nje ya nchi, wanarithi hali hii. Na hakika, haki ya "kurudi" katika maeneo ambayo sasa ni ya Israeli, kama ilivyoainishwa na sheria za kimataifa.

Hata hivyo, idadi hii ya wakimbizi imeongezeka mara nne katika miaka 50 na sasa inafikia karibu watu milioni 6. Kwa hivyo Israeli hofu, ambayo pia inaungwa mkono hapa na Washington. Balozi wa Marekani tayari ametoa wito wa "mageuzi" ya UNRWA, wakati ukaguzi huru utatangazwa Jumatatu Aprili 22.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.