Pata taarifa kuu
SYRIA-UNSC-USALAMA

Baraza la Usalama kupiga kura kuhusu uchunguzi wa silaha za kemikali Syria

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamia kuamua wakati wa kura Jumanne hii kama wataongeza au la muda wa uchunguzi kuhusu mashambulizi ya silaha za kemikali nchini Syria, wanadiplomasia walisema siku ya Jumatatu Oktoba 23.

Kwenye lango la kijiji cha Khan Cheikhoun nchini Syria, Julai 12, 2017, kijiji kilicholengwa na mashambulizi ya gesi aina ya sarin mwezi Aprili 2017.
Kwenye lango la kijiji cha Khan Cheikhoun nchini Syria, Julai 12, 2017, kijiji kilicholengwa na mashambulizi ya gesi aina ya sarin mwezi Aprili 2017. AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inaweza kukamishwa kwa kura ya turufu ya Urusi, mshirika wa serikali ya Rais Bashar al-Assad, anayetaka kushauriana kabla ya ripoti hii kutolewa siku ya Alhamisi kuhusu mashambulizi kemikali aina ya sarin mwezi Aprili katika kijiji cha Cheikhoun Khan, ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 80.

Marekani ilikuwa ilitoa wito wa kupiga kura kuhusu rasimu ya azimio iliyowasilishwa wiki iliyopita ili kuwezesha kamati ya wataalam wa Umoja wa Mataifa na OPCW (Shirika la linalopiga marufuku silaha za kemikali) kuendelea kwa mwaka mwingine na kazi zao kubaini wahusika wa mashambulizi ya silaha za kemikali katika kipindi cha miaka sita ya vita nchini Syria.

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley alitoa wito siku ya Ijumaa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kuchukua hatua sasa" kwa kuunga mkono kuongezwa kwa muda huo.

Muhula wa sasa wa Kamati ya Uchunguzi iliyopewa jina la Joint Investigation Mechanism (JIM) - inamaliza muda wake tarehe 18 Novemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.