Pata taarifa kuu
IRAN

Raia wa Iran kupiga kura siku ya Ijumaa kumchagua rais mpya

Raia Milioni 55 wa Iran watapiga kura siku ya Ijumaa, kumchagua rais mpya.

Mkutano wa kisiasa nchini Iran
Mkutano wa kisiasa nchini Iran Reuters
Matangazo ya kibiashara

Huu ni uchaguzi wa 12 wa urais nchini humo, utawashirikisha pia wapiga kura wengine Milioni 2.5 watakaopiga kura katika mataifa 103 ikiwa ni pamoja na Marekani.

Ni uchaguzi unaoangaziwa kwa karibu sana na wachambuzi wa siasa katika eneo la Mashariki ya Kati na Mataifa ya Magharibi ambayo kwa muda mrefu  yamekuwa na uhusiano mgumu kutokana na mradi wa Nyuklia wa Iran.

Iran ni taifa lenye nguvu katika eneo la Mashariki ya Kati, na udhabiti wake wa kisiasa utaathiri hatima ya kisiasa ya nchi jirani kama Syria, Yemen na Iraq ambayo yameendelea kukabiliana na changamoto za kiusalama.

Rais Hassan Rouhani ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 akiwa na ajenda ya mabadiliko, alifanikiwa kufikia mwafaka kuhusu mradi wa Nyuklia, atamenyana na wagombea wengine watatu.

Wagombea hao ni pamoja na Ebrahim Raisi, Mostafa Mir-Salom na Mostafa Hashemitaba.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa rais Rouhani ana nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kutokana na ungwaji mkono wa vyama vidogo nchini humo lakini anakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa Ebrahim Raisi.

Kueleka Uchaguzi huo, Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya mradi wake wa Nyuklia, hatua ambayo Tehran inasema huenda ikaathiri mkataba uliotiwa saini mwaka 2015 na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.