MATTIS;Iran ni mfadhili mkuu wa ugaidi duniani
Waziri wa ulinzi wa Marekani James Mattis amesema hii leo kuwa Iran ni taifa kubwa linalofadhili ugaidi duniani wakati huu Rais wa Marekani Donald Trump akiiwekea vikwazo Iran kufuati hatua yake ya hivi karibuni ya kufanya jaribio kombora.
Imechapishwa:
Waziri huyo wa ulinzi wa Marekani ameyasema hayo katika mkutano na vyombo vya habari mjini Tokyo akidai Marekani haina mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi wake katika eneo la mashariki ya kati.
Aidha raisi Trump aliandika kwenye mtandao wa twitter kuwa,Iran inacheza na moto, hawana shukran jinsi Obama alikuwa mkarimu kwao, Si mimi!"
Lakini utawala wa Iran unasema kuwa hauwezi kulegeza kamba kutokana na vitisho visivyo na maana vya Marekani, kutoka kwa mtu asiye na ujuzi.