Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Iran: mwanasayansi anyongwa kwa maslahi ya Marekani

Mwanasayansi wa nyuklia wa Iran amenyongwa nchini Iran, baada ya kutuhumiwa kufanya upelelezi kwa maslahi ya marekani, zaidi ya miaka mitano baada yakukabiliwa na kesi ya ajabu iliyohusika na madai ya kutekwa nyara na Idara ya upelelezi ya Marekani (CIA).

Mwanasayansi wa Iran Shahram Amiri, Julai 14, 2010 mjini Tehran.
Mwanasayansi wa Iran Shahram Amiri, Julai 14, 2010 mjini Tehran. AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran bado inaichukulia Marekani kama "adui" yake mkuu na Kiongozi mkuu Ali Khamenei ameua akirejelea kauli yake ya kutokua na "imani" na Marekani licha ya kufufua uhusiano wao hivi karibuni katika neema ya mkataba wa mwaka 2015 juu ya mpango wa nyuklia wa Iran uliyozua utata.

mauaji ya Shahram Amiri, mwenye umri wa miaka 39, ambaye alikua hajulikani alipo tangu mwaka 2010, yametangazwa Jumapili na msemaji wa mahakama ya Iran, Gholamhossein Mohseni-Ejeie, katika mkutano na waandishi wa habari.

"Mtu huyu alikuwa akipokea kiurahisi taarifa zote za siri muhimu za serikali na alianzisha mahusianona adui yetu mkuu, Shetani mkuu, Marekani. Alikua akimpa adui taarifa muhimu za siri za nchi" amesema Mohseni-Ejeie.

"Amiri alinyongwa," amesemaMohseni-Ejeie, bila kufafanua wapi au wakati gani alinyongwa.

Mwanasayansi wa Iran alitoweka mwezi Juni 2009 nchini Saudi Arabia ambapo alikuwa katika Hija. Alionekana mwezi Julai mwaka 2010 nchini Marekani akiomba kurudi Iran. Wakati huo alikuwaalipokelewa kwa mikono miwili na serikali ya Iran.

Bw Mohseni-Ejeie almesema Amiri alihukumiwa "adhabu ya kifo na mahakama ya mwanzo, kulingana na sheria." Alikata rufaa "lakini Mahakama Kuu ilizingatia hukumu" ya kifo.

"Siyo tu kujirubisha lakini alijaribu kutuma taarifa za uongo kutoka ndani ya gereza, na hatimaye aliadhibiwa," Bw Mohseni-Ejeie ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.