Pata taarifa kuu
SYRIA

Waasi wa Syria watishia kutoshiriki mazungumzo ya Astana

Makubaliano ya kusitisha mapigano nchini Syria yako hatarini kuvunjika wakati huu vikosi vya Serikali vikiongeza mashambulizi jirani na mji wa Damascus, na tayari makundi 10 ya waasi yametangaza kuahirisha kushiriki kwenye mazungumzo ya amani yaliyopangwa kufanyika mwezi huu. 

Askari wakipita kwenye viunga vya mji wa Aleppo nchini Syria hivi karibuni.
Askari wakipita kwenye viunga vya mji wa Aleppo nchini Syria hivi karibuni. REUTERS/Khalil Ashaw
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo haya yanatarajiwa kufanyika katika mji mkuu wa Kazakhistan, Astana, mwishoni mwa mwezi Januari, lakini waasi wamesema wanajiondoa kutokana na Serikali kukiuka makubaliano ya usitishaji wa mapigano mjinu Damascus.

Mazungumzo haya yanaratibiwa na Urusi, ambayo inaunga mkono utawala wa Syria huku Iran na Uturuki zenyewe zikiwaunga mkono waasi.

"Wakati huu ukiukaji wa makubaliano ukiendelea kushuhudiwa, upande wa waasi unatangaza kusitisha mazungumzo yote yanayoratibiwa mjini Astana," imesema taarifa ya pamoja ya waasi.

Waasi wa Syria wamesema kuwa "waliheshimu mkataba wa usitishaji mapigano nchi nzima, lakini utawala wa Damascus na washirika wake hawajaacha kushambulia na wameanzisha operesheni kubwa na mara nyingi tu wamekiuka makubaliano ya amani.

Kwa majuma kadhaa yaliyopita, hata kabla ya kuanza kwa utekelezwaji wa nchi nzima kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Uturuki na Urusi, vikosi vya Serikali vimekuwa vikiendesha mashambulizi ya anga kwenye mji wa Wadi Barada, ulioko umbali wa kilometa 15 kutoka Damascus.

Jumatatu ya tarehe 2, jeshi la Syria likisaidiwa na mashambulizi ya anga, limesonga mbele kuendelea kuchukua maeneo zaidi, ambayo ni muhimu kwa usambazaji wa maji katika jiji kuu la Damascus, imesema taarifa ya shirika la kibinadamu nchini Syria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.