Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO-USALAMA

Mashambulizi ya angani na mapigano vyashuhudiwa Syria

Ndege za kivita za Syria ziliendesha mashambulizi ya angani Jumapili hii Januari 1 katika maeneo kadhaa ya Syria ambako mapigano yaliendelea kushuhudiwa hasa karibu na mji wa Damascus, licha ya mkataba wa usitishwaji wa mapigano uliosainiwa Ijumaa usiku wa manane, shirika la haki za Binadamu nchini Syria (OSDH) na vyanzo vya waasi vimearifu.

Mapigano yaendelea kurindima katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Syria.
Mapigano yaendelea kurindima katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Syria. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa OSDH mashambulizi kadhaa ya angani yalishuhudiwa katika vijiji vya Kafr Kar, Mintar na karibu na mji wa Banan, kusini mwa mji wa Aleppo. OSDH pia imesema kuwa mashambulizi ya angani yalishuhudiwa katika milima ya Wadi barada, eneo lililo karibu na mji wa Damascus linaloshikiliwa na waasi.

Karibu na mji mkuu, pia, vikosi vya serikali vimesonga mbele dhidi ya waasi mashariki mwa eneo la Ghouta Mashariki. Mashamba makubwa kumi yaliyo karibu na mji wa Duma yametekwa na wapiganaji, OSDH imesema.

Hata hivyo hali ya utulivu imeshuhudiwa katika mikoa mingine ya Syria, ambako mapigano yalikua yakiendelea siku za hivi karibuni.

Gazeti lenye mafungamano na kundi la Hezbollah, mshirika wa rais Bashar al Assad, limebaini kwamba jeshi la Syria liliharibu gari la kivita la kundi la zamani la al Nosra Front katika mkoa wa kusini mwa mji wa Aleppo.

Jeshi limesema kuwa kundi la waasi linalojulikana kwa jina la Fatah al Sham Front na tawi la Al Qaeda nchini Syria, halihusiki katika mkataba wa usitishwaji wa mapigano lakini waasi wanasema vinginevyo.

Mkataba wa usitishwaji wa mapigano, uliyoandaliwa na Urusi pamoja na Uturuki, ulikaribishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambapo siku ya Jumamosi ulipitisha kwa kauli moja azimio linalokaribisha mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.