Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Urusi kupiga kura yake ya turufu kuhusu azimio la waangalizi Aleppo

Urusi imetangaza kwamba itapiga kura ya turufu kuhusu rasimu ya azimio la Umoja wa Mataifa linalopanga kutumwa kwa waangalizi kwa ajili ya kuwaondoa raia katika mji wa Aleppo nchini Syria, amesema Jumapili balozi wa Urusi.

Raia na wapiganaji wa upinzani nchini Syria wakisubiri kuondolewa kutoka eneo la waasi la Aleppo Mashariki, Desemba 16, 2016.
Raia na wapiganaji wa upinzani nchini Syria wakisubiri kuondolewa kutoka eneo la waasi la Aleppo Mashariki, Desemba 16, 2016. REUTERS/Abdalrhman Ismail
Matangazo ya kibiashara

"Hatuwezi kuruhusu kura nakala hiyo ipigiwe kwa sababu ni janga," amesema Vitaly Churkin.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana Jumatatu Desemba 19 ili kupiga kura kuhusu azimio hilo saa 5:00 mchana 11:00 (sawa na 10:00 saa za kimataifa).

Bw Churkin ameongeza kuwa Urusi, mshirika muhimu wa serikali ya Syria ya Bashar al-Assad, atapendekeza rasimu yake binafsi ya kutumwa kwa waangalizi katika mji wa Aleppo, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Urusi tayari imeshapiga kura ya turufu kwa maazimio sita kuhusu Syria tangu kuanza kwa mgogoro ambao umeababisha vifo vya watu zaidi ya 310,000 tangu Machi 2011.

Azimio la Ufaransa linapendekeza kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon kutuma haraka mjini Aleppo wafanyakazi wa kutoa misaada wa Umoja wa Mataifa ambao wapo mjini Syria "kwa uchunguzi wa kutosha usioegemea na uangalizi wa moja kwa moja " kwa kuondoa raia katika maeneo yanayoshikiliwa katika mji mkoa wa Aleppo".

Hayo yakijiri mabasi kadhaa yameanza kuingia Jumapili hii katika maeneo ya waasi ili kuendelea na zoezi la kuwaondoa maelfu ya raia na waasi wanaokabiliwa na njaa.

Inaarifiwa kuwa watu 40,000 ndio wanaosalia na kati ya wapiganaji 1,500 hadi 5,000 na familia zao bado wapo eneo hili, kwa mujibu wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Staffan de Mistura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.