Pata taarifa kuu
SYRIA-USALAMA

Assad awapongezaWasyria kwa "ukombozi" wa Aleppo

Rais wa Syria Bashar al-Assad amekaribisha Alhamisi hii Desemba 15 ushindi wa askari wake katika mji wa Aleppo na kusema Syria "imeandika historia" kwa kuwatimua waasi katika mji wa pili wa nchi ya Syria.

Rais wa Syria awapongeza wananchi wake kwa ushindi wa askari wake mjini Aleppo.
Rais wa Syria awapongeza wananchi wake kwa ushindi wa askari wake mjini Aleppo. SANA/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Hayo yakijiri mabasi ishirini na magari ya wagonjwa kumi yanatumiwa katika zoezi la kuwahamisha wakazi wa mji wa Alepo nchini Syria kiwa ni pamoja na waasi pamoja familia zao, Waziri wa Ulinzi wa Urusi amebaini.

Kufuatia makubaliano kati ya serikali na waasi, watu waliojeruhiwa na familia zao ndio wameanza kuondoka na kisha waasi na familia zaopamoja na "wanamgambo 250" wasiokuwa na silaha wanapinga serikali, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

Aidha, chanzo hicho kimesema, watu waliojeruhiwa na wagonjwa kutoka Foua na Kefraya, vijiji viwili vinavyokaliwa na Mashia wengi ambavyo vinadhibitiwa nawaasi katika mkoa jirani wa Idleb, pia watahamishwa katika maeneo yanayoshikiliwa na serikali.

Wapiganaji 12000 na familia zao pia zoezi hilo linawahusu.

Kudhibitiwa kwa Aleppo na jeshi la serikali itakua pigo kubwa kwa waasi ambao walidhibiti sehemu ya mashariki ya mji wa pili wa Syria mwaka 2012, lakini leo wanajikuta wameangamizwa baada ya mashambulizi makali ya jeshi la serikali yaliyozinduliwa katikati mwa mwezi Novemba.

Umoja wa Mataifa wasimamia na kusaidia" zoezi la kuwahamisha waasi

Umoja wa Mataifa umesemakuwa uliombwa "kusimamia na kusaidia zoezi la kuwaondoa watu waliojeruhiwa, wasiojiweza na wapiganaji."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.