Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA-HAKI

Polisi ya Burundi yakanusha kuhusika katika visa vya utekaji nyara

Jeshi la Polisi nchini Burundi limekanusha kuhusika na kukamatwa kwa mmoja wa viongozi wa upinzani wa chama cha UPD Leopold Habarugira anayedaiwa kutekwa nyara na watu waliokuwa wamevalia mavazi ya jeshi la Polisi.

Polisi wapiga doria katika moja ya mtaa wa Bujumbura, Aprili 12, 2016.
Polisi wapiga doria katika moja ya mtaa wa Bujumbura, Aprili 12, 2016. STRINGER / cds / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye amesema polisi hawahusiki kwa vyovyote na utekaji wa watu nchini Burundi na wala haikuagiza kukamatwa kwa kiongozi huyo.

Akizungumza na idhaa hii mke wa Haba-ru-gira, Liberate Nzitonda ameleza kuhusu namna mume wake alivyochukuliwa na watu wasiofahamika.

Leopold Habrugira, ambaye ni kada wa chama cha upinzani cha UPD-ZIgamibanga alikamatwa siku ya Jumanne asubuhi alipokua akifanya mazoezi asubuhi karibu na chuo kikuu cha wauguzi mjini Bujumbura.

Visa vya utekaji nyara vimekithiri nchini Burundi. Mashirika ya haki a binadamu yanabaini kwamba watu zaidi ya 1,000 wametekwa katika kipindi kisichozidi mwaka mmoja.

Mashirika hayo yameenyooshea kidolea chalawama baadhi ya maafisa wa idara ya ujasusi na vijana kutoka chama tawala CNDD-FDD, Imbonerakure, kuhusika na vitendo hivyo dhidi ya wanasiasa na wafuasi wa vyama vya upinzani. Yametaja hata baadhi ya askari na polisi wanaotumiwa katika vitendo hivyo.

Tukio hili limekuja ikiwa ni juma moja tu limepita toka kutolewa kwa ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoitaja Serikali ya Burundi kuhusika na vitendo vya utekaji nyara na mauaji ya raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.