Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-SIASA-HAKI

Kesi ya ung'atuzi dhidi ya Trump: Maseneta watafoutiana

Kesi ya kumwondoa madarakani, rais wa Marekani Donald Trump imeanza mbele ya Kamati ya baraza la Senate. Katika mchakato huu, nafasi ya urais ya bwana Trump iko mashakani.

Rais Trump anakabiliwa na mashtaka mawili: kutumia vibaya madaraka yake na kudharau mamlaka ya bunge.
Rais Trump anakabiliwa na mashtaka mawili: kutumia vibaya madaraka yake na kudharau mamlaka ya bunge. REUTERS/Yuri Gripas
Matangazo ya kibiashara

Kesi ya kumshtaki rais wa Marekani Donald Trump ilifunguliwa Jumannre wiki hii, ukiwa ni mchakato muhimu kuhusu ikiwa aondolewe madarakani kufuatia kitendo chake cha kuishinikiza Ukraine ianzishe uchunguzi dhidi ya mpinzani wake wa kisiasa kutoka chama cha Democratic pamoja na hatua ya kuzuia bunge kumchunguza.

Maseneta wa chama cha Republican na Democratic, wametofautiana vikali kuhusu utaraibu wa kufuatwa kuhusu kesi hii.

Maseneta wa chama cha Democratic wanasema ushadhidi mpya, kukubaliwa katika kesi hii, kwa kile wanachosema itasaidia pakubwa kutenda haki katika kesi hiyo.

Hata hivyo, mawakili wa rais Trump wanasema madai ya Maseneta wa Democratic yanaonesha kuwa, hakuna ushahidi dhidi ya mteja wao.

Kwa sasa nchi kwa ujumla imegawika kwa kiasi kikubwa ikiwa ni wiki kadhaa kabla ya kinya'nganyiro cha uchaguzi wa awali wa kutafuta mgombea wa chama cha Democrats.

Rais Trump anakabiliwa na mashtaka mawili katika baraza hilo, kutumia vibaya madaraka yake na kudharau mamlaka ya bunge, madai ambayo rais Trump amekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.