Pata taarifa kuu
VENEZUELA-MAZUNGUMZO-USALAMA-SIASA

Venezuela: Upinzani na serikali wakubaliana kuhusu mazungumzo

Serikali na upinzani nchini Venezuela wamekubaliana kuanzisha mfumo wa mazungumzo ya kudumu, serikali ya Norway imesema katika taarifa yake.

Kiongozi wa upinzani Juan Guaidó na rais Nicolás Maduro.
Kiongozi wa upinzani Juan Guaidó na rais Nicolás Maduro. Fuente: AFP.
Matangazo ya kibiashara

"Mfumo umeanzishwa na utafanya kazi kwa kasi na kwa haraka, ili kufikia suluhisho la mazungumzo na kwa uwezekano unaotolewa na Katiba," Wizara ya Mambo ya Nje ya Norway imesema katika taarifa iliyotolewa leo Ijumaa mjini Caracas.

"Inatarajiwa kwamba pande husika zitaendelea na majadiliano ili kuendeleza mazungumzo," Wizara ya ya Mambo ya Nje ya Norway imeongeza, bila kutoa tarehe kuhusu mazungumzo mapya.

Serikali ya Norway imehimiza pande zote mbili kuchukua "tahadhari kwa kutoa maoni na taarifa zao kuhusiana na mchakato" wa mazungumzo.

"Ninasema tena shukrani zangu kwa pande zote mbili kwa juhudi zao na roho ya ushirikiano na ninaishukuru Serikali ya Barbados kwa ukarimu wake," Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Ine Eriksen Søreide amesema katika taarifa hiyo.

Serikali na upinzani wamekuwa wakikutana tangu Jumatatu (Julai 8) katika mji wa Barbados kwa kikao cha tatu cha mazungumzo tangu Mei, yakiongozwa chini ya upatanishi wa Norway. Mikutano miwili ya kwanza iliyofanyika huko Oslo mwezi Mei haikuzaa matunda yoyote.

Vyanzo vkutoka pande zote mbili vimethibitishia shirika la Habari la AFP kumalizika wa mazungumzo katika mji wa Barbados.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.