Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Watu maarufu kufadhili maandamano dhidi ya silaha Marekani

Watu wengi maarufu nchini Marekani, ikiwa ni pamoja na George Clooney, Oprah Winfrey na Steven Spielberg wametangaza kuwa kila mmoja atatoa dola laki 5 kuandaa "Maandamano kwa kuhofia Maisha ya Watu" yatakayofanyika mwezi ujao mjini Washington kwa minajili ya kutaka udhibiti mkubwa wa silaha.

Waigizaji wa filamu na wanamuziki maarufu kama Steven Spielberg (kwenye picha) wako tayari changia fedha zao kwa kusaidia kudhibiti silaha nchini Marekani.
Waigizaji wa filamu na wanamuziki maarufu kama Steven Spielberg (kwenye picha) wako tayari changia fedha zao kwa kusaidia kudhibiti silaha nchini Marekani. REUTERS/Eduardo Munoz
Matangazo ya kibiashara

George na Amal Clooney walikuwa wa kwanza kutoa mchango wao kwa umma na kutangaza kuwa watashiriki katika maandamano ambayo yatafanyika katika mpango huo, ikiwa ni pamoja na waathirika wa mashambulizi katika shule ya sekondari ya Parkland, katika jimbo la Florida, ambapo wanafunzi 17 wa shule ya sekondari waliuawa na aliyekuwa mwanafunzi katika shule hiyo wiki moja iliyopita.

"Familia yetu itakuwa hapo Machi 24 ili kuungana na kizazi hiki cha vijana kutoka kote nchini na kwa niaba ya watoto wetu, Ella na Alexander, tunatoa dola laki 5 kusaidia kufadhili tukio hili la msingi. Maisha ya watoto wetu yanategemea tukio hili, "amesema Clooney katika taarifa yake.

Mtayarishaji wa filamu Steven Spielberg na mkewe, Kate Capshaw, muigiizaji wa filamu Jeffrey Katzenberg na Oprah Winfrey wameahidi kutoa mchango huo.

"Hawa vijana msukumo wao kukumbuka Freedom Riders ya miaka ya 1960 ambao walikuwa pia alisema walikuwa na ya kutosha na kwamba wangeweza kusikika," aliandika Oprah Winfrey kwa ajili yake Twitter.

Watu wengine maarufu ambao wamesema wanaunga mkono maandamanohayo ni wanamuziki Justin Bieber, Lady Gaga na Cher.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.