Pata taarifa kuu
MAREKANI-SIASA

Wajumbe 270 kuamua mshindi wa urais nchini Marekani

Uamuzi wa mwisho wa mshindi wa urais nchini Marekani huamuliwa na wajumbe 538 wanaoteuliwa kutoka katika majimbo yote 50 nchini humo.

Wagombea urais nchini Marekani Donald Trump (Kushoto) na Hillary Clinton (Kulia)
Wagombea urais nchini Marekani Donald Trump (Kushoto) na Hillary Clinton (Kulia) REUTERS/Carlo Allegri (L)/Carlos Barria (R)/File Photos
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii huja mara baada ya raia wa kawaida kupiga kura katika vituo mbalimbali na kumchagua rais wao wanaotaka awaongoze kwa muda wa miaka minne.

Mgombea anastahili kupata angalau kura 270 za wajumbe kati ya 538 ili kuwa rais wa Marekani na wajumbe hao huamua mshindi kwa namna watu walivyopiga kura katika majimbo mbalimbali.

Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2012, Barrack Obama alipata ushindi baada ya kuchaguliwa kwa kupata kura 65,915,795 huku mpinzani wake Mitt Romney akipata kura 60,933,504.

Wajumbe walipopiga kura, Obama alipata ushindi wa wajumbe 332 dhidi ya Romney aliyepata kura ya wajumbe 206 katika uchaguzi huo.

Wajumbe walicyopiga kura wakati wa Uchaguzi wa Mwaka 2012
Wajumbe walicyopiga kura wakati wa Uchaguzi wa Mwaka 2012

Kuelekea Uchaguzi huu, kuna majimbo ambayo ni ngome ya chama cha Republican sawa na Democratic lakini kuna majimbo mengine kama Florida, Pennsylvania na Ohio ambayo hayana mwenywe, hayo ndio majimbo ambayo yataamua mshindi wa uchaguzi huu.

Pamoja na kumchagua rais siku ya Jumanne, raia wa Marekani watapiga kura kuwachagua wawakilishi 435 wanaohudumu kwa miaka miwili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.