Pata taarifa kuu
UN-CAR-UBAKAJI

Ubakaji wa watoto CAR: UN yashindwa dhahiri kujitetea

Kundi la wataalamu huru limesema Alhamisi hii "kushindwa dhahiri" kwa Umoja wa Mataifa katika usimamizi wa mashtaka ya ubakaji wa watoto uliofanywa na askari wa Ufaransa na wale kutoka Afrika nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa karibu kata ya PK5 mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati wa ziara ya Papa Francis, Novemba 10, 2015.
Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa karibu kata ya PK5 mjini Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati wa ziara ya Papa Francis, Novemba 10, 2015. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

"Matokeo ya mwisho yalikuwa ni kushindwa dhahiri kwa upande wa Umoja wa mataifa kwa kujibu shutuma hizo kwa kiasi kikubwa", imebainisha ripoti ya kikundi cha wataalamu watatu chini ya uenyekiti wa Jaji kutoka Canada Marie Deschamps.

"Njia ambayo mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliitikia mashtaka haya iligubikwa na kasoro kubwa", ripoti hiyo imeongeza.

Ripoti hiyo ya kurasa mia moja, ambayo ilikua ikisubiriwa kwa hamu na gamu, inabaini kwamba kuna mapungufu katika taasisi hiyo ya kimataifa katika mji wa Bangui pamoja na viongozi waandamizi mjini Geneva na New York baada ya kesi hiyo kuwekwa wazi.

Ripoti hii inamkosoa hasa mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MiINUSCA), Babacar Gaye, raia wa Senegal, ambaye alijiuzulu mwezi Agosti.

Pia inawakosoa viongozi wa UNICEF mjini Bangui na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu kwa kutowasilisha shutma za ubakaji kwa viongozi wao wakuu, au kutochukua haraka hatua za kutosha kwa kulinda au kusaidia watoto.

"Taarifa kuhusu mashtaka haya zilipita kutoka ofisi kwenda nyingine (...) hakuna mtu ambaye alitaka kuchukua jukumu kwa ajili ya kuwatendea haki waathirika wa ubakaji huo, ambapo ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu", inasema ripoti hiyo.

Katika taarifa yake ndefu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ambaye aliliteua jopo hilo la wataalamu mwezi Juni, amesema "amezingatia yaliyomo katika ripoti hiyo" na kuahidi kuchukua hatua kali "bila kuchelewa ".

Alielezea "masikitiko yake kuona watoto hao walisalitiwa na watu ambao walitumwa kuwalinda."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.