Pata taarifa kuu

Urusi kuzindua kampeni ya kujiandikisha katika jeshi katika msimu wa joto

Urusi itazindua kampeni yake ya kujiandikisha katika jeshi katika msimu wa joto siku ya Jumatatu ambayo itahusu makumi ya maelfu ya vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 30, makao makuu ya jeshi la Urusi ilitangaza siku ya Ijumaa Machi 29. Warusi wengi wanaogopa wimbi la pili la uhamasishaji, wakati askari 617,000 wa Urusi tayari wako nchini Ukraine.

Askari wa jeshi la Urusi na kifaru wakati wa maonyesho ya silaha huko Saint Petersburg, Februari 24, 2024 (picha ya kielelezo).
Askari wa jeshi la Urusi na kifaru wakati wa maonyesho ya silaha huko Saint Petersburg, Februari 24, 2024 (picha ya kielelezo). AP - Dmitri Lovetsky
Matangazo ya kibiashara

"Kampeni ya kujiandikisha kijeshi ya msimu wa joto itaanza Aprili 1," afisa Mkuu wa katika makao makuu ya jeshi, Vladimir Tsimlianski, alisema katika mkutano mfupi. Kampeni iliyoandaliwa mara mbili kwa mwaka.

Lakini jeshi linahakisha kwamba wanajeshi  hawa wapya hawatatumwa Ukraine. Kulingana na Vladimir Tsimlianski, wanajeshi wote wapya mara baada ya kusajiliwa watafanya kazi yao, kwa muda wa mwaka mmoja, kwenye "ardhi ya Shirikisho la Urusi". "Hawatatumwa kwa vituo vya kupelekwa kwa vikosi vya jeshi katika majimbo mapya ya Urusi", ambayo ni majimbo manne ya Ukraine (yale ya Donetsk, Lugansk, Kherson na Zaporizhia) yaliyoshikiliwa na Urusi mnamo mwaka 2022, na "hawatashiriki katika Operesheni maalum ya kijeshi ya Urusi, Vladimir Tsimlianski amebainisha.

Hofu

Urusi imekuwa ikiongoza mashambulizi nchini Ukraine kwa zaidi ya miaka miwili, ambayo tayari yamesababisha mamlaka ya Urusi kuamuru uhamasishaji wa watu zaidi ya 300,000 katika msimu wa mwaka 2022. Warusi wengi wanaogopa wimbi la pili la uhamasishaji, licha ya uhakikisho kutoka kwa Rais Vladimir Putin, aliyechaguliwa tena Machi, kwamba "sio lazima".

Mnamo mwaka 2023, kampeni ya kujiandikisha kijeshi la msimu wa joto ilihusisha watu wapatao 147,000 nchini Urusi, kampeni ya msimu wa vuli walijiandikisha wanajeshi wapya 130,000 wakijiunga na jeshi la Urusi, kulingana na Wizara ya Ulinzi. Haijulikani ni vijana wangapi wa Urusi wanaolengwa na kampeni ya masika mwaka huu. Msimu uliopita wa kiangazi, Urusi ilipitisha sheria ya kuongeza kikomo cha umri wa kujiandikisha kutoka miaka 27 hadi miaka 30 kuanzia Januari 1, 2024.

Maendeleo kadhaa nchini Ukraine

Katika miezi ya hivi karibuni, Urusi imedai maendeleo kadhaa nchini Ukraine, ambayo inakabiliana na jeshi la Ukraine lililokosa watu na risasi kutokana na kukosa msaada wa nchi za Magharibi. Mwezi wa Desemba mwaka uliyopita, Vladimir Putin alisema katika mkutano wake wa kila mwaka na waandishi wa habari kwamba wanajeshi 617,000 wa Urusi walikuwa nchini Ukraine kama sehemu ya operesheni ya kijeshi ya Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.