Pata taarifa kuu

Wales: Vaughan Gething kuchukuwa nafasi ya Waziri Mkuu ajaye

Nchini Uingereza, kila taifa linaloundwa lina serikali na bunge lake, linalojiendesha kwa mambo fulani. Kiongozi wa sasa wa chama cha Labour Mark Drakeford amejiuzulu na atakabidhi madaraka mwishoni mwa mwezi huu. Vaughan Gething anatarajia kuchukuwa mikoba ya mtanulii wake.

Bendera za Wales au Muungano, mbele ya jengo la bunge la Wales huko Cardiff, mnamo 2022 (picha ya kielelezo).
Bendera za Wales au Muungano, mbele ya jengo la bunge la Wales huko Cardiff, mnamo 2022 (picha ya kielelezo). AFP - GEOFF CADDICK
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Uingereza, Émeline Vin

Vaughan Gething ambaye alizaliwa Zambia, atakuwa kiongozi wa kwanza mweusi kote Ulaya. Wakili huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 50, mtoto wa daktari wa mifugo wa Wales na mama yake ambaye ni mfugaji wa kuku kutoka Zambia, amechaguliwa Jumamosi hii Machi 16 kama kiongozi wa chama cha Labour cha Wales na kwa hivyo atachukua uongozi wa taifa la Uingereza.

Katika hotuba yake ya ushindi, Vaughan Gething amesifu "ukurasa unaofunguliwa katika kitabu cha nchi yetu". Familia yake ililazimika kuondoka Wales alipokuwa mtoto kwa sababu ya ubaguzi wa rangi.

Ingawa amejihusisha na siasa tangu ujana, mbunge tangu mwaka 2011, wakazi wa Wales walimjua Vaughan Gething wakati wa janga la UVIKO; wakati huo alikuwa Waziri wa Afya, ambaye tanu wakati huo alihamia Uchumi.

Kampeni yake ilitatizwa na ufadhili wa mfanyabiashara aliyepatikana na hatia ya uharibifu wa mazingira.

Ushindi wake katika uchaguzi wa ndani wa Chama cha Wafanyikazi cha Wales, ambao uliwaleta pamoja wapiga kura chini ya 100,000 kati ya watu milioni 3, ulikaribishwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak, lakini sio na watu wanaotaka kujitenga wa Wales.

Bunge la Wales sasa lazima limuidhinishe Vaughan Gething kuchukuwa nafasi ya mkuu wa serikali katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.