Pata taarifa kuu

Uingereza: Mpango wa kuwatuma wakimbizi Rwanda wakabiliwa na mgawanyiko

Nairobi – Waziri mkuu wa Uingereza,  Rishi Sunak  ameendelea kushuhudia mgawanyiko  kutoka kwa chama chake cha Conservative kuhusu mpango wa kuanzisha tena sheria mpya ya kuwatuma watafuta hifadhi nchini Rwanda.

Mpango huo umekuwa ukikabiliwa na upinzani
Mpango huo umekuwa ukikabiliwa na upinzani © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sunak ambaye ameufanya mpango wa kuwapeleka watafuta nchini Rwanda kipao mbele chake, anapata pingamizi kutoka kwa baadhi ya wabunge wa chama chake ambao wanadai, Sunak anafahamu fika kwamba mpango huo hautafulu.

Hata hivyo zaidi ya wabunge 30 wa mrengo wa kulia wanaunga mkono sheria ya Sunak, kutaka kufanya vigumu yeyote kufika mahakamani kupinga watafuta hifadhi hao kusafirishwa hadi nchini Rwanda.

Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza lazima mpango huo utaendelea
Waziri mkuu wa Uingereza amesisitiza lazima mpango huo utaendelea © AFP - Ben Stansall

Waziri wa zamani wa uhamiaji ambaye alijiuzulu mwezi uliopita Robert Jenrick ,na amabye anaongoza uasi dhidi ya sheria mpya, amesema sheria hiyo haitazuia watu kufika mahakama kupinga mpango huo ambao mahakama ya juu tayari ilisema ni kinyume cha sheria.

Baadhi ya wabunge hata hivyo wanadai kwamba Sunak ameshikwa mateka na chama chake hasa baada ya madai kuibuka kwamba alipinga mpango huo wakati  akihudumu katika wizara ya fedha.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu.
Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakipinga mpango huo wakisema unakiuka haki za binadamu. © Getty Images

Uingereza inalenga kuwatuma watafuta hifadhi nchini Rwanda, na kuweka sheria inayozuia wahamiaji kuingia nchini humo kiholela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.