Pata taarifa kuu

Msaada kwa Ukraine: Ufaransa, Ujerumani na Poland zaonyesha umoja wao

Baada ya kuonyesha hadharani tofauti katika mkakati wa kuidhinisha kuunga mkono Ukraine, Ufaransa na Ujerumani zimetaka kuonyesha umoja wao. Ili kuimarisha ujumbe huu, mkutano katika muundo unaoitwa "Weimar" umefanyika siku ya Ijumaa Machi 15 karibu na Kansela Scholz huko Berlin, pamoja na Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk.

Emmanuel Macron, Olaf Scholz na Donald Tusk - viongozi watatu wa pembetatu ya Weimar - huko Berlin mnamo Machi 15, 2024.
Emmanuel Macron, Olaf Scholz na Donald Tusk - viongozi watatu wa pembetatu ya Weimar - huko Berlin mnamo Machi 15, 2024. AFP - ODD ANDERSEN
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Berlin, Pascal Thibaut

"Moja kwa wote, wote kwa moja": viongozi watatu wa pembetatu ya Weimar wamesherehekea umoja wao katika uungaji mkono wao thabiti kwa Ukraine siku ya Ijumaa.

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ametaja ugomvi wa Ufaransa na Ujerumani wa wiki za hivi karibuni kuwa wa kukadiria: "Mkutano wa leo unaonyesha wazi kwamba uvumi fulani mbaya wa tofauti kati ya miji mikuu ya Ulaya umepita kipimo," amebaini  mkuu wa serikali ya Poland.

Olaf Scholz alizungumza kuhusu mazungumzo siku ya Alhamisi na Rais Zelensky: "Anajua anaweza kututegemea," amehakikisha.

Emmanuel Macron, ambaye matamshi yake juu ya uwezekano wa vikosi vya ardhini nchini Ukraine yaliikasirisha sana Berlin, ametoa ishara kwa Ujerumani kwa kukataa "mpango wowote wa kuongezeka kwa uhasama".

Olaf Scholz amekariri: "Hatuko vitani na Urusi. "

Kansela ametangaza kuanzishwa kwa muungano wa washirika wa Ukraine ili kutoa silaha za masafa marefu kwa Ukraine. Nia ya kununua silaha nje ya Ulaya ikiwa ni lazima imethibitishwa. Na faida kutoka kwa mali ya Urusi iliyohifadhiwa Ulaya itatumika kufadhili ununuzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.