Pata taarifa kuu

Ukraine: Idadi ya vifo kufuatia shambulio la Urusi Odessa yaongezeka hadi 14

Shambulio la kombora la Urusi limesababisha vifo vya watu 14 na 46 kujeruhiwa siku ya Ijumaa huko Odessa, mji wa bandari kusini mwa Ukraine, kulingana na ripoti mpya iliyorekebishwa na kuwasilishwa na gavana wa jimbo hilo, Oleg Kiper.

Majengo ya makazi na magari yameharibiwa na shambulio la Urusi katika jimbo la Odessa, kulingana na ofisi ya mwendesha mashitaka wa Ukraine.
Majengo ya makazi na magari yameharibiwa na shambulio la Urusi katika jimbo la Odessa, kulingana na ofisi ya mwendesha mashitaka wa Ukraine. AFP - OLEKSANDR GIMANOV
Matangazo ya kibiashara

"Shambulio la kombora la Urusi limeua watu 14, wakiwemo wakaazi, mhudumu wa afya na afisa wa jeshi la Zimamoto na uokoaji ," gavana wa jimbo hilo, Oleg Kiper, amesema kwenye Telegram, na kuongeza kuwa watu wengine 46 wmejeruhiwa, wakiwemo wafanyikazi saba wa idara ya huduma ya dharura.Β 

Majengo ya makazi na magari yameharibiwa na shambulio hilo, kulingana na ofisi ya mwendesha mashitaka wa Ukraine.

Hayo yanajiri wakati Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrel alionya jana kwamba mustakabali wa vita vya Ukraine huenda ukajulikana katika miezi ijayo na kuwahimiza washirika kuongeza kasi ya kupeleka misaada nchini humo.

Borrel aliwaambia waandishi wa habari akiwa ziarani mjini Washington kwamba amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake yote juu ya athari kwa Ukraine ikiwa Urusi itashinda vita hivyo.

Alisema, kama Rais Vladimir Putin atashinda na kuweka vibaraka wake kama alivyofanya nchini Belarus, ni wazi kuwa harakati zake hazitaishia hapo na kutaka misaada kupelekwa haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.