Pata taarifa kuu

Maeneo kadhaa ya Urusi yalengwa na mashambulio ya ndege za Ukraine

Shambulio jipya la ndege zisizo na rubani limelenga eneo la nishati nchini Urusi leo Jumatano Machi 13, ambalo limelengwa kwa siku ya pili mfululizo kutoka Ukraine, kitendo ambacho Vladimir Putin ameshutumu kwa kutaka kudhoofisha uchaguzi wa urais nchini Urusi.

Rais Vladimir Putin wakati wa mahojiano na kituo cha Rossia 1 mnamo Machi 12, 2024.
Rais Vladimir Putin wakati wa mahojiano na kituo cha Rossia 1 mnamo Machi 12, 2024. via REUTERS - Gavriil Grigorov
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limelenga kiwanda cha kusafisha mafuta huko Ryazan, karibu kilomita 200 kusini mashariki mwa Moscow. “Kiwanda cha kusafisha mafuta cha Ryazan kilishambuliwa na ndege isiyo na rubani [...]. Kulingana na habari za awali, kuna watu waliojeruhiwa, "gavana wa mkoa wa Ryazan, Pavel Malkov, ameandika kwenye Telegram leo Jumatano asubuhi. Kulingana na gavana huyo, kufuatia shambulio hilo, "moto ulizuka" katika kiwanda hiki cha kusafishia mafuta, mmoja wa wazalishaji wakubwa wa mafuta katikati mwa Urusi na kusimamiwa na kampuni kubwa ya mafuta ya Rosneft. Ndege nyingine isiyo na rubani ilidunguliwa siku ya Jumatano ilipokaribia kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Leningrad, karibu na St Petersbourg, amebaini gavana wa jimbo hilo, Alexandre Drozdenko.

Shambulio hili linakuja siku mbili kabla ya uchaguzi uliopangwa nchini Urusi kutoka Machi 15 hadi 17, ambao utamfanya bwana wa Kremlin kushinda kwa muhula mwingine wa miaka sita, bila kuwepo na upinzani wowote.

Kwa jumla, ndege zisizo na rubani 58 zililenga maeneo kadhaa ya Urusi wakati wa usiku na asubuhi, haswa yale ya Belgorod, Briansk, Kursk na Voronezh, yote manne ambayo yanapakana na Ukraine, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Wizara ya Ulinzi ya Urusi, kuhakikisha kuwa yote yaliharibiwa. .

"Kuhujumu uchaguzi"

Maeneo kadhaa ya Urusi, haswa yale ya Belgorod na Kursk yanayopakana na Ukraine, yanalengwa na mashambulio mengi ya ndege zisizo na rubani za Ukraine kwa siku ya pili mfululizo, na maeneo ya nishati kwenye njia panda.

Rais wa Urusi Vladimir Putin Jumatano ameishutumu Ukraine kwa kushambulia maeneo ya Urusi katika jaribio la kuhujumu uchaguzi wa urais. Mashambulizi haya yanaweza kuelezewa "kwa urahisi sana. Haya yote yanatokea dhidi ya hali ya kushindwa katika uwanja wa vita,” Vladimir Putin alisema katika mahojiano na kituo cha Rossia 1 na shirika la habari la Ria Novosti, sehemu zake ambazo zilirushwa hewani Jumatano asubuhi. "Hata hivyo, lengo kuu, sina shaka, ikiwa watashindwa kudhoofisha uchaguzi wa urais nchini Urusi, angalau ni kujaribu kuzuia raia kwa njia fulani kuelezea nia yao," rais wa Urusi amehakikisha.

Tusk atangaza mkutano wa kilele kuhusu Ukraine na Poland, Ujerumani na Ufaransa siku ya Ijumaa

Viongozi wa Poland, Ujerumani na Ufaransa watakutana Ijumaa mjini Berlin kwa mkutano wa dharura utakaohusu Ukraine, Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ametangaza. "Siku ya Ijumaa, nitakuwa Berlin na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz kujadili hali hiyo," amesema Donald Tusk, wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha umma cha TVP Info kilichorusha mahojiano hayo siku ya Jumanne jioni, baada ya mkutano wake na Rais wa Marekani Joe Biden huko Washington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.