Pata taarifa kuu

Sumatra (Indonesia) yakumbwa na mafuriko, kumi wafariki na 10 hawajulikani waliko

Mafuriko na maporomoko ya ardhi yamesababisha vifo vya takriban watu 10 na wengine wengi kutoweka kwenye kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia, afisa wa eneo hilo amesema Jumamosi kulingna na shirika la utangazaji la ubelgiji la RTBF.

"Watu kumi walikutwa wamefariki" katika wilaya tofauti za mkoa huo, Doni Yusrizal, kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa maafa wa Pesisir Selatan, amesema katika taarifa.
"Watu kumi walikutwa wamefariki" katika wilaya tofauti za mkoa huo, Doni Yusrizal, kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa maafa wa Pesisir Selatan, amesema katika taarifa. Basarnas/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mvua kubwa imesababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi katika wilaya ya Pesisir Selatan ya mkoa wa Sumatra Magharibi, na kuwalazimu karibu watu 46,000 kutafuta makazi katika makazi ya muda.

"Watu kumi walikutwa wamefariki" katika wilaya tofauti za mkoa huo, Doni Yusrizal, kaimu mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa maafa wa Pesisir Selatan, amesema katika taarifa.

Watu wengine kumi hawajulikani waliko, ameaini, akiongeza kuwa hali mbaya ya hewa ilifanya zoezi la kutafuta manusura na miili zaidi kuwa mgumu.

Zaidi ya nyumba 20,000 zakumbwa na mafuriko

Takriban nyumba 14 zilisombwa na maporomoko ya ardhi, zaidi ya nyumba 20,000 zimejaa maji na madaraja manane yameporomoka, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.

Bado katika Sumatra Magharibi, lakini katika wilaya nyingine, ile ya Padang Pariaman, mvua kubwa iliyonyesha kati ya Alhamisi na Ijumaa ilisababisha mito kufurika na kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi na kuua watu wasiopungua watatu, kulingana na taarifa nyingine.

Maporomoko ya ardhi hutokea mara kwa mara nchini Indonesia wakati wa msimu wa mvua unaoendelea sasa. Tatizo limefanywa kuwa mbaya zaidi katika baadhi ya maeneo kutokana na ukataji miti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.