Pata taarifa kuu

Tetemeko jipya la ardhi nchini Uturuki, katika mkoa wa Hatay ambao tayari umeathiriwa vibaya

Tetemeko jipya la ardhi, la ukubwa wa 6.4 kwenye kipimo cha Richter, limepiga Jumatatu Februari 20, 2023 katika eneo la kusini mwa Uturuki ambalo tayari liliathiriwa vibaya na tetemeko la hivi karibuni.

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.4 limepiga kusini mwa Uturuki mnamo Februari 20, 2023.
Tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.4 limepiga kusini mwa Uturuki mnamo Februari 20, 2023. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Kitovu cha tetemeko hilo kiko katika eneo la Defne katika mkoa wa Hatay. Tetemeko hilo limetokea saa 8:04 usiku kwa saa za nchini Uturuki (sawa na saa 5:04 jioni saa za kimataifa).

Kulingana na timu za shirika la habari la AFP, tetemeko hili jipya la ardhi limepiga huko Antakya (Antiokia), kama dakika kumi na tano kutoka kwa kitovu kwa mwendo wa gari katika nyakati za kawaida, lakini pia huko Adana, kilomita 200 kaskazini ikilinganishwa na eneo la Defne.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa shirika la habari la AFP, tetemeko hilo limezua hofu miongoni mwa watu waliokuwa tayari wameathiriwa vibaya, na kurusha mawingu makubwa ya vumbi katika mji huo ulioathiriwa.

Almeona na kusikia sehemu kadhaa za kuta za jengo ambazo tayari zilikuwa zimeharibiwa vibaya zikibomoka na watu kadhaa, waliojeruhiwa, wakiomba msaada.

Kulingana na Mamlaka ya Kudhibiti Maafa na Dharura ya Uturuki (AFAD) , zaidi ya mitetemeko 6,000 imerekodiwa tangu tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lililoathiri kusini mwa Uturuki na Syria.

Taarifa zaidi zinakujia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.