Pata taarifa kuu

Kashfa baada ya ufichuzi wa uuzaji wa mahema kwa shirika lisilo la kiserikali Ukraine

Wiki tatu baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.8 lililoharibu kusini-mashariki mwa Uturuki, zaidi ya watu milioni moja wameachwa bila makaazi. Mwandishi wa habari za uchunguzi Murat Agirel amefichua katika gazeti la kila siku la upinzani Cumhuriyet kwamba Shirika la Hilali Nyekundu la Uturuki liliuza mahema kwa shirika lisilo la kiserikali la Ahbap kwa euro milioni 2.3.

Des équipes de secours d'urgence cherchent des personnes sous les reVikosi vya uokoaji vya dharura vinawatafuta watu walio chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa katika mji wa Nurdagi, viunga vya mji wa Osmaniye, kusini mwa Uturuki, Jumanne, Februari 7, 2023.stes de bâtiments détruits dans la ville de Nurdagi, à la périphérie de la ville d'Osmaniye, dans le sud de la Turquie, mardi 7 février 2023.
Des équipes de secours d'urgence cherchent des personnes sous les reVikosi vya uokoaji vya dharura vinawatafuta watu walio chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa katika mji wa Nurdagi, viunga vya mji wa Osmaniye, kusini mwa Uturuki, Jumanne, Februari 7, 2023.stes de bâtiments détruits dans la ville de Nurdagi, à la périphérie de la ville d'Osmaniye, dans le sud de la Turquie, mardi 7 février 2023. AP - Khalil Hamra
Matangazo ya kibiashara

Habari hizo zilisababisha wimbi la hasira kwenye mitandao ya kijamii, ambalo lilitafsiriwa haraka mitaani kwa wito wa Chama cha Wafanyakazi cha Uturuki. Takriban watu 100 walikusanyika nje ya eneo la Hilali Nyekundu ya Uturuki, upande wa Asia wa Istanbul,

Haluk Levent, msanii na mwanzilishi wa NGO ya Ahbap, alikiri kununua mahema 15,250, ambayo 2,500 yalinunuliwa kutoka Kizilay, Hilali Nyekundu ya Uturuki, siku ya 3 baada ya tetemeko la ardhi, wakati wa kilele cha janga la kibinadamu.

Mamlaka ya Uturuki imetoa wito wa kuchangia kwa  shirika la Hilali Nyekundu nchini Uturuki. Kizilay, kama AFAD, shirika la kukabiliana na tetemeko la ardhi, limekuwa likikosolewa vikali tangu kuanza kwa mgogoro wa afya.

Vyombo vya habari huru na upinzani vinakosoa misimamo inayohusishwa na wale walio karibu na AKP badala ya wataalamu wenye uwezo katika nyanja za misaada ya kibinadamu.

Kutokuwa na imani kunaongezeka kidogo dhidi ya mamlaka ya Uturuki, huku uchaguzi wa urais na wabunge uliopangwa kufanyika Mei 14, utafanyika kwa tarehe walioafikiana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.